Kiini cha atomu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Atomi lithi.jpg|thumbnail|Muundo wa atomi kwa mfano wa lithi: Mzingo wa Elektroni na Kiini cha atomi katika kitovu chake. Kiini kinafanywa na nyutroni (bila chaji) na protoni (chaji chanya).]]
'''Kiini cha atomi''' (pia '''nyukliasi ya atomiatomu'''; kwa [[Kiingereza]] ''atomic nucleus'') ni sehemu ya ndani ya [[atomi]] inayozungukwa na [[mzingo elektroni]].
 
Atomi ni chembe ndogondogo kabisa zinazounda na kutofautisha [[elementi]] mbalimbali. Kila [[maada]] imeundwa na chembechembe ndogo za aina moja zinazojulikana kama [[molekyuli]]. Hizi molekyuli huwa ni muungano wa [[elementi]] za aina moja au aina tofauti ("kampaundi": kutoka Kiingereza "compounds"). Chembe ndogo ya kila elementi huitwa [[atomu]]. Kila elementi ina atomu za aina yake kulingana na asili yake. Ndani ya kila atomu kuna chembechembe za aina tofauti, mojawapo ikiwa [[kiini]] chake.
 
[[Kiini]] kinaundwa na [[protoni]] na [[nyutroni]]<ref>isipokuwa katika atomi ya [[hidrojeni]] ambayo ni atomi ndogo kabisa, ina protoni 1 pekee katika kiini</ref> na hizi kwa pamoja huitwa "nyukleoni" <ref>kutoka [[lat.]] nucleus = kiini, yaani chembe za kiini</ref>.
Line 16 ⟶ 18:
 
==Ugunduzi==
Ugunduzi wa [[nadharia ya atomu]] na wa kuwa ndani yake kuna [[elektroni]] ulileta maswali mengi ambayo hayakupatiwa majibu. Atomu ilijulikana [[kiumeme]] kuwa haikuwa na [[chaji]] ya aina yoyote, lakini chembe cha [[elektroni]] zilizomo ndani ya atomu zilijulikana kuwa na [[chaji hasi]] za [[umeme]]. Hivyo lazima ndani ya atomu (ambayo haina chaji) kutakuwa na chaji aina nyingine (ambayo ni lazima iwe [[chaji chanya]]) ambayo inaletwa uwiano sawa wa kuifanya atomu kutokuwa na chaji. Fumbo gumu zaidi lilikuwa ni kwa namna gani hizo aina mbili za chaji zinaweza kuwa zimejipanga ndani ya atomu.
Kuwepo kwa kiini ndani ya atomi kulitambuliwa mwaka [[1911]] na [[Ernest Rutherford]] aliyefanya majaribio ya kufyatulia [[mnururisho wa alfa]] dhidi ya bati nyembamba ya [[dhahabu]].
[[Picha:Atomic structure.gif |thumb|350px|right|Muundo wa atomi]]
=== Muundo wa J. J. Thomson ===
Mawazo ya kwanza kabisa kuhusu muundo wa atomu yalitoka kwa [[J.J. Thomson]]. [[Mwanasayansi]] huyu alipendekeza kuwa atomu ni kama [[mpira]] ambao katika kuta zake una chaji chanya zenye ukubwa sawa na zile za hasi ambazo zinaelea ndani ya mpira. Hii ina maana kama utaweza kufikiria kuweza kuingiza [[mkono]] katika atomu na kama una bahati unaweza kutoa elektroni ndani ya atomu.
 
Muundo huu uliweza kuelezea kwa nini atomu hazina chaji, lakini ulishindwa kujibu maswali mengi yaliyotokana na [[nadharia]] nyingine nyingi ambazo zilikuwa zimethibitishwa, hasa zile za [[umeme]] na [[usumaku]].
 
=== Namna nyukliasi ilivyogunduliwa ===
Muundo wa atomu wa J. J. Thomson haukuwa na nyukliasi. Mwaka [[1909]] [[H. Geiger]] na [[E. Marsden]] walichapisha matokeo ya mlolongo wa majaribio waliyofanya katika [[chuo kikuu cha Manchester]] chini ya uongozi wa [[Ernest Rutherford]]. Rutherford alikuwa na mvuto mkubwa juu ya [[sayansi]] ya [[mionzi ya radioaktiviti]] ambayo ilianzishwa na [[Becquerel]] na [[Curies]].
 
Mojawapo ya mafumbuzi ya kwanza yalikuwa kwamba elementi zilitoa [[chembe za alfa]] (α-particles). Chembe za alfa ziligundulika kuwa na vitu viwili vilivyokuwa na chaji chanya, na vilibainika kuwa ni atomu za [[Helium]] zilizopoteza elektroni [[mbili]]. Hivyo chembe alfa zilikuwa ni [[ayoni]] za Helium, He<sup>2+</sup>.
 
Geiger na Marsden walielekeza mkondo wa chembe alpha katika foili nyembamba ya [[metali]]. Waligundua kuwa chembe zilibadilishiwa njia kwa ukubwa wa nyuzi mbalimbali kutoka ile njia ya awali. Suala la kubadilishwa njia walikuwa wanalitegemea lakini kilichowashangaza ni kiwango cha badiliko la njia. Baadhi zilibadilishwa hadi kufikia nyuzi 150⁰ (nyuzi 180⁰ ni sawa na kuzuiliwa kabisa kupita).
 
Kutokana na matokeo iliochenya kuwa ni sehemu ndogo sana ya chembe alfa ndizo zilizobadilishwa njia kwa nyuzi nyingi. Lakini la msingi hapa si uchache wake, bali ni nini kilisababisha hii [[tabia]] isiyotarajiwa.
 
Kuwepo kwa kiini ndani ya atomi kulitambuliwa mwaka [[1911]] na [[Ernest Rutherford]] aliyefanya majaribio ya kufyatulia [[mnururisho wa alfa]] dhidi ya bati nyembamba ya [[dhahabu]]. Yeye alionyesha kuwa atomu zenye chaji chanya zilizotawanya katika kuta zake kama vile alivyofikiri J. J.Thompson zisingeweza kubadili njia kwa nyuzi ndogo. Mabadiliko makubwa ya uelekeo ya chembe chanya yangeweza kutokea kama kungekuwa na mkusanyiko mdogo ndani ya atomu. Rutherford alionyesha kwa kutumia [[dhahabu]] kuwa ndani ya atomu kulikuwa na mkusanyiko wa chaji uliosababisha yote hayo. Alisema ungekuwa ndani ya tufe au mpira wenye [[nusu kipenyo]] kisichozidi [[mita]] 3.2 × 10<sup>-14</sup>. Kwa atomu nyingine zilizokuwa nyepesi zaidi ya dhahabu, nusu kipenyo ilipungua hadi kufikia mita 3 × 10<sup>-15</sup>.
 
Wakati huo, nusu kipenyo cha atomu kilikuwa kimekadiriwa kwenye mita 2 × 10<sup>-10</sup>, hivyo haikuchukua muda kuona kuwa chaji chanya ndani ya atomu zitakuwa ndani ya tufe ambalo nusu kipenyo chake ni kama mara 10000 hadi 100000 ya nusu kipenyo cha atomu yote.
 
Kwa maneno mengine, Rutherford, Geiger na Marsden walikuwa wameanzisha nadharia kuwa atomu zina [[nyukliasi]] ndani yake.
 
Ugunduzi wa [[nadharia ya atomu]] na wa kuwa ndani yake kuna [[elektroni]] ulileta maswali mengi ambayo hayakupatiwa majibu. Atomu ilijulikana [[kiumeme]] kuwa haikuwa na [[chaji]] ya aina yoyote, lakini chembe cha [[elektroni]] zilizomo ndani ya atomu zilijulikana kuwa na [[chaji hasi]] za [[umeme]]. Hivyo lazima ndani ya atomu (ambayo haina chaji) kutakuwa na chaji aina nyingine (ambayo ni lazima iwe [[chaji chanya]]) ambayo inaletwa uwiano sawa wa kuifanya atomu kutokuwa na chaji. Fumbo gumu zaidi lilikuwa ni kwa namna gani hizo aina mbili za chaji zinaweza kuwa zimejipanga ndani ya atomu.
 
=== Ugunduzi wa protoni ===
[[Picha:Mass Spectrometer Schematic.svg |thumb|400px|left|[[Mass Spectrometer]]]]
Ilikuwa imejulika kuwa chaji chanya, zinazoifanya atomu kutokuwa na chaji hata kama kuna chaji za elektroni, zilikuwa zinapatikana ndani ya nyukliasi. Hivyo hizi chaji ndani ya nyukliasi ziliaminika kutoka ndani ya chembechembe zilizokuja kufahamika kama [[protoni]]. Kwa kuwa atomu haina chaji, basi chaji ya protoni ni sawa kabisa na ile ya elektroni isipokuwa yenyewe ni chanya na ile ya elektroni ni hasi.
 
Njia iliyotumika katika kuthibitisha uwepo wa protoni ni kifaa kilichoitwa [[mass spectrograph]]. Muundaji wa kifaa hiki alikuwa [[F. W. Aston]]. Katika kifaa chake, atomu zilizochajiwa chanya zilipitishwa katika [[eneo la usumaku]]. Eneo hili liliundwa ili kuleta atomu zenye [[tungamo]] tofautitofauti kwenye [[filamu]]. Wakati filamu ilipoboreshwa, mistari ingeweza kuonekana kulingana na ayoni zilivyoifikia. Kwa jinsi Aston alivyounda kifaa chake ilimaanisha mistari ingekuwa katika umbo la [[parabola]].
 
Suala msingi kuhusu kifaa hicho (mass spectrograph) ni kuwa njia inayopitiwa na ayoni inapinda wakati ikisafiri katika eneo la usumaku. Kupinda huku kunategemea vitu wiwili: chaji ya ayoni, q, na tungamo lake, m. Ayoni iliyokuwa na uwiano sawa wa chaji kwa tungamo, [[q/m]] zitawasili katika sehemu kwenye filamu. Kwa kufanya jaribio hili kwa uangalifu na [[hisabati]], Aston aliweza kupima uwiano wa chaji kwa tungamo wa idadi kubwa ya ayoni.
 
Kutokana na matokeo aliunda “kanuni ya namba ya jumla“. Kutokana na kanuni hii uwiano wa chaji na tungamo wa kila ayoni ulikuwa mara kadhaa ya ule wa ayoni za [[Hydrojeni]]. Ilionyesha Hydrojeni kuwa ni ayoni iliyojenga ayoni (na atomu) nyingine. Hivyo jina protoni, kutoka neno la [[Kigiriki]] ‘[[protos]]’ ikimaanisha ‘ya kwanza’, ilipewa ayoni ya hydrojeni.
 
=== Ugunduzi wa neutroni ===
Miongoni mwa matokeo ya majaribio ya Aston kuna kwamba tungamo la atomu ya [[oksijeni]] ilikuwa mara 16 zaidi ya lile la protoni. Kufuatia ugunduzi wa Rutherford wa nyukliasi, na uchunguzi wa Moseley wa namba ya atomu, ilikuwa wazi kuwa nyukliasi ya oksijeni ina chaji chanya [[nane]] tu. Hii ilimaanisha ina protoni nane, lakini tungamo la oksijeni lilionyesha kuwa kubwa (karibia mara mbili zaidi) kuliko protoni nane.
 
Utata huo uliondolewa na [[James Chadwick]] mwaka [[1932]] kwa ugunduzi wa [[neutroni]].
Ilichukua muda mrefu tangu majaribio ya Aston (1919) hadi ugunduzi wa neutron (1932). Sababu iliyopelekea kuwa hivi ni kutokuwepo kwa chaji katika neutroni, hivyo kufanya kuwa vigumu kugundulika kwa kutumia usumaku au umeme.
 
Msingi wa ugunduzi wa Chadwick ulikuwa kama ifuatavyo. Aliweka [[chanzo]] cha chembe za alpha kwenye upande mmoja wa foili ya [[beryllium]]. Upande mwingine wa beryllium kulikuwa na [[kinasa chembe]] (detector) cha alpha ambacho kiligundua uwepo wa ayoni. Katika mpangilio huu, ayoni hazikuweza kugundulika katika kinasa chembe. Kisha [[mche]] wa [[paraffin]] uliwekwa katikati ya beryllium na kinasa chembe, hali iliyopelekea kinasa chembe kugundua uwepo wake. Hivyo lazima kutakuwa na chembechembe zilizotoka katika beryllium na kusababisha [[pambano]] ambalo lilipelekea ayoni kugundulika katika kinasa chembe za ayoni. Hizi chembechembe zilikuja kugundulika kuwa ni neutroni.
 
Baada ya kugundua kuwepo kwa nyutroni mwaka [[1932]] [[Dmitri Ivanenko]] alitunga maelezo ya kiini cha atomi kuwa nyutroni na protoni <ref>{{cite journal|author=Iwanenko, D.D.|title= The neutron hypothesis|journal= Nature |volume=129|issue= 3265|pages= 798|doi=10.1038/129798d0|year= 1932|bibcode = 1932Natur.129..798I }}</ref> na [[Werner Heisenberg]].<ref>{{cite journal |last=Heisenberg |first=W. |title=Über den Bau der Atomkerne. I |journal=[[Z. Phys.]] |volume=77 |pages=1–11 |year=1932 |doi=10.1007/BF01342433 |bibcode = 1932ZPhy...77....1H }}</ref><ref>{{cite journal |last=Heisenberg |first=W. |title=Über den Bau der Atomkerne. II |journal=Z. Phys. |volume=78 |pages=156–164 |year=1932 |doi=10.1007/BF01337585 |issue=3–4 |bibcode = 1932ZPhy...78..156H }}</ref><ref>{{cite journal |last=Heisenberg |first=W. |title=Über den Bau der Atomkerne. III |journal=Z. Phys. |volume=80 |pages=587–596 |year=1933 |doi=10.1007/BF01335696 |issue=9–10 |bibcode = 1933ZPhy...80..587H }}</ref><ref>Miller A. I. ''Early Quantum Electrodynamics: A Sourcebook'', Cambridge University Press, Cambridge, 1995, ISBN 0521568919, pp. 84–88.</ref><ref>{{cite book |author1=Fernandez, Bernard |author2=Ripka, Georges |lastauthoramp=yes |title=Unravelling the Mystery of the Atomic Nucleus: A Sixty Year Journey 1896 — 1956 |chapter=Nuclear Theory After the Discovery of the Neutron |chapterurl=https://books.google.com/books?id=4PxRBakqFIUC&pg=PA263 |year=2012 |publisher=Springer |isbn=9781461441809 |page=263 }}</ref>
Line 28 ⟶ 70:
Kwa hali ya kawaida atomi haionyeshi [[chaji ya umeme]]. Ina chaji ndani yake kulingana na idadi ya protoni ambazo ni chanya na elektroni ambazo ni hasi. Katika hali ya kawaida idadi yake ni sawa, kwa hiyo chaji zinabatilishana. Lakini kama elektroni zinaondoka katika mzingo elektroni hali inabadilika na atomi huonyesha chaji. Kiini cha atomi peke yake daima kina chaji chanya maana hakina elektroni zilizomo katika mzingo.
 
=== Namba ya atomu ===
==Marejeo==
Uthibitisho kuwa chaji chanya katika nyukliasi zilikuwa chembe za msingi na muhimu ulitolewa na [[H. G. J. Moseley]]. Katika majaribio yake ya mwaka [[1913]] katika [[chuo kikuu cha Manchester]], Moselay aligongesha elementi kadhaa na [[mionzi ya cathode]] (elektroni). [[Nishati]] iliyotolewa na mionzi ilisababisha elementi kutoa [[mionzi X]]. Moselay alichunguza uhusiano kati ya [[mizunguko]] (frequency) ya mionzi X na asili ya elementi iliyokuwa inaitoa. Kwa njia hiyo Moselay aliweza kuonyesha kuwa [[namba ya atomu]]], ambayo ilikuwa inafahamika kama idadi ya protoni katika nyukliasi, ilipelekea mpangilio wa elementi katika [[Jedwali la Elementi]] ([[Mfumo radidia]]).
 
=== Ulinganifu wa elektroni, protoni na neutroni ===
Tungamo la protoni lilikuwa kwa kiasi fulani rahisi kupima kwa kutumia mass spectrograph. Hata hivyo njia hii haiwezi kutumika kupima tungamo la neutroni. Badala yake, neutroni ziligongeshwa na chembe nyingine za atomu. [[Mwendokasi]] na tungamo za chembe zilizotolewa (emitted) zilipimwa. Kwa kutumia [[kanuni ya utunzaji wa momentamu]] (The Law of Conservation Momentum), iliwezekana kukokotoa tungamo la neutroni. Tungamo la neutroni lilibainika kuwa karibu sawa na lile la protoni. Angalia jedwali hapa chini.
{| class="wikitable"
|-
! chembe
! tungamo (kg)
! chaji
! uwiano wa chaji kwa tungamo (C/kg)
|-
| elektroni
| 0.00091 x 10<sup>-27</sup>
| hasi (-)
| -1.758820150 x 10<sup>11</sup>
|-
| neutroni
| 1.6749 x 10<sup>-27</sup>
| haina chaji
| 0
|-
| protoni
| 1.6726 x 10<sup>-27</sup>
| chanya (+)
| 9.5788339 x 10<sup>7</sup>
|}
 
== Hitimisho ==
Ni muhimu kufahamu kuwa ingawa atomu imeundwa na chembechembe tofauti, yenyewe kwa jumla haina chaji ya aina yoyote. Hii ni kwa sababu atomu zina idadi sawa ya protoni (chaji chanya) na elektroni (chaji hasi). Idadi ya neutroni (haina chaji) katika nyukliasi ya atomu si lazima iwe sawa na idadi ya protoni au elektroni. Tofauti hiyo ya neutroni katika nyukliasi za atomu ya elementi moja hupeleka kuwa na [[isotopes]] za elementi.
Elektroni hutembea kuzunguka nyukliasi ya atomi. Ikiwa atomi ina chaji, hii ni kwa sababu imepata (na kuwa na chaji hasi) au imepoteza (na kuwa chaji chanya) elekroni; lakini si kwa sababu idadi yake ya protoni imebadilika.
 
== Angalia pia ==
* [[atomu]]
* [[elektroni]]
* [[muundo wa atomu]]
 
==Tanbihi==
<references/>
 
== Marejeo ==
Atkins, P. W. (1990). Physical Chemistry, Oxford University Press, Oxford.<br />Matthews, P. S.C. (1986). Quantum Chemistry of Atoms and Molecules, Cambridge Unversity Press, Cambridge.<br />Matthews, P. (2003). Advanced Chemistry, Cambridge Unversity Press, Cambridge.
 
== Viungo vya nje ==
* [http://www.syvum.com/cgi/online/serve.cgi/squizzes/chem/atomic1.html Kemia : Atomu na Muundo wa Atomu]
* [http://www.slideshare.net/guest5c8bc1/history-of-atomic-structure Historia ya Muundo wa Atomu]
* [http://nobeliefs.com/atom.htm Historia ya Atomu]
 
{{mbegu-kemia}}