52,022
edits
No edit summary |
|||
Mstari 108:
==Mpira wa miguu barani Afrika==
Mchezo ulipelekwa Afrika na Waingereza wakati wa ukoloni. Mechi za kwanza zilizorekodiwa mwaka 1862 huko [[Cape Town]] na [[Port Elizabeth]]<ref>[http://www.nytimes.com/2010/06/10/sports/soccer/10iht-SRHISTORY.html C. Clarey, Soccer Returns to Its Roots in Africa] New York Times 9-06-2010, iliangaliwa 6-12-2016</ref>.
Ilhali ulikuwa mwanzoni mchezo wa kizungu ulienea haraka kati ya vijana Waafrika kupitia shule, jeshi na wafanyakazi wa reli. Kwa mfano kisiwani [[Unguja]] walikuwa wafanyakazi Wazungu na Wahindi waliocheza soka pamoja wakitazamiwa na wenyeji, halafu wanafunzi wa shule ya misioni St Andrew's ya [[UMCA]]. Khamis Fereji alikumbuka jinsi gani mnamo 1910 soka ilichezewa na watoto na vijana kote Zanzibar mjini wakitumia mipira ya tennis mtaani au mwambanoni wakati wa jioni ilhali wazee walitazama. Vivyi hivyo aliandika Dr. Nmandi Azikiwe katika kumbukumbu ya maisha yake ya kwamba alipokuwa mtoto Calabar (Nigeria) kabla ya Vita Kuu ya Kwanza walicheza mpira kila mahali kwa kutumia maembe, machungwa au mipira ya tennis<ref>[https://books.google.de/books?id=NrW50yHkr0EC&printsec=frontcover&dq=African+Soccerscapes:+How+a+Continent+Changed+the+World%27s+Game&hl=en&sa=X&redir_esc=y#v=onepage&q=African%20Soccerscapes%3A%20How%20a%20Continent%20Changed%20the%20World%27s%20Game&f=false Peter Alegi, African Soccerscapes: How a Continent Changed the World’s Game ] uk. 6. ilitazamiwa kupitia google books tarehe 9-12-2016</ref>
Mchezo ukaendelea kupanuka na kuendeshwa na wenyeji katika klabu zilizoundwa wakati miji ilikua na kuwa na wakazi wengi Waafrika<ref>.Alegi u. 18</ref>.
Tangu uhuru soka ilipanuka sana katika nchi huru za Afrika. Baada ya kujiunga na [[FIFA]] wawakilishi wa nchi huru za Afrika waliweza kuhakikisha ya kwamba Afrika Kusini ilitengwa kwa sababu ya siasa yake ya [[apartheid]] (ubaguzi wa rangi).
Tangu 1970 mpango wa kombe la dunia ulibadilishwa kuhakikisha nafasi kwa kila bara na Afrika ilipewa nafasi 1 ya hakika. 1986 zilikuwa nafasi 2, 1998 nafasi 4 na tangu kombe la 2002 kuna nafasi 5 kwa timu kutoka Afrika. <ref>[http://exploringafrica.matrix.msu.edu/football-soccer-in-africa Soccer in Africa], iliangaliwa 9-12-2016</ref>
Kwa [[Tanzania]] na nchi nyingi za [[Afrika]] kuna uhaba wa [[wafadhili]]ː hiyo husababisha [[timu]] ambazo hazina uwezo wa kiuchumi kukata tamaa. Tatizo kubwa ni uhamisho wa wachezaji vijana wenye uwezo kuhamia nje ya Afrika. Wakati wa kombe la dunia idadi kubwa wachezaji wa timu za kitaifa kutoka Afrika wanaajiriwa na klabu huko Ulaya; wakati wa kombe la dunia dunia 2010 walikuwa asilimia 80 za wachezaji Waafrika kwenye kombe la dunia waliocheza kwa klabu za Ulaya. Hali hii inashusha uwiano wa soka katika ligi za kitaifa kwa sababu wachezaji bora wako ng'ambo wakipatikana tu kwa mechi za kimataifa wakishiriki katika timu ya kitaifa.<ref>[http://www.npr.org/templates/story/story.php?storyId=127600200 Mahojiano na profesa Peter Alegi], npr.org tar. 9-06-2010, ikiangaliwa tarehe 9-12-2016</ref>
==Mpira wa miguu nje ya kanuni za kawaida==
|