Leopold Sedar Senghor : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{Infobox officeholder |name = Léopold Sédar Senghor |image = Léopold Sédar Senghor.jpg |office = Rais wa kwanza wa Senegal |ter...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 01:10, 12 Desemba 2016

Léopold Sédar Senghor (9 Oktoba 1906 – 20 Disemba 2001) alikuwa mshairi, mwanasiasa na rais wa kwanza wa Senegal kati ya 1960 na 1980 .

Léopold Sédar Senghor


Rais wa kwanza wa Senegal
Muda wa Utawala
6 Septemba 1960 – 31 Disemba 1980
Waziri Mkuu Abdou Diouf
mtangulizi Office created
aliyemfuata Abdou Diouf

tarehe ya kuzaliwa (1906-10-09)9 Oktoba 1906
Joal, Afrika ya Magharibi ya Kifaransa (leo Senegal)
tarehe ya kufa 20 Desemba 2001 (umri 95)
Verson, Ufaransa
chama Chama cha Kisoshalisti cha Senegal
ndoa Ginette Éboué (1946-1956)
Colette Hubert Senghor (m. 1957–2001) «start: (1957)–end+1: (2002)»"Marriage: Colette Hubert Senghor to Leopold Sedar Senghor" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Leopold_Sedar_Senghor);hadi kifo
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Paris
dini Kanisa Katoliki
signature

Senghor alikuwa Mwafrika wa kwanza aliyechaguliwa kuwa mwanachama wa Académie française. Kabla ya uhuru aliunda chama cha Umoja wa Kidemokrasia wa Senegal (fr.: Bloc démocratique sénégalais; ing.: Senegalese Democratic Bloc). Wengi wanamhesabu kati ya wataalamu muhimu zaidi Waafrika katika karne ya 20.

Maisha

Senghor alizaliwa katika kijiji cha Joal kilichowahi kuwa kati ya vituo vya kwanza vya wafanyabiashara wa Ulaya na pia kitovu cha misioni ya kikatoliki kwenye pwani la Senegal. Babake alikuwa mfanyabiashara mzalendo, mamaye mke wa tatu wa baba na Mislamu.

Alipokuwa na miaka 8 alianza kUsuoma shule ya mapadre akaendelea kwenye seminari ya mapadre wa Roho Mtakatifu na baadaye alishauriwa asiendelee kutafuat masomo ya upadre alisoma shule ya kawaida. Alimaliza vema hasa kwa masomo ya Kifaransa na Kilatini akapewa nafasi ya kusoma chuo Ufaransa [1].

1928 Senghor alienda Ufaransa aliposoma lugha [2] na baadaye sarufi ya Kifaransa kweye Chuo Kikuu cha Paris. Baada ya masomo alipewa nafasi ya kufundisha kwenye vyuo vya Tours na Paris. 1932 aliwahi kupata uraia wa Ufaransa.

Tangu siku zake masomoni alikuwa na urafiki na Aime Cesaire na pamoja naye alibuni hoja la "negritude" walipotetea kuwepo kwa utamaduni wa pekee wa "watu weusi" kama utamaduni wa pekee na muhimu tofauti na utamaduni wa Kiulaya.

Mwaka 1945 baada ya vita na uhuru wa Ufaransa alijiunga na chama cha kisoshalisti akachaguliwa kama mbunge.

1960 alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Senegal akaendela kushika naafsi hii hadi 1980.

Marejeo

  1. Bryan Ryan. Major 20th-Century Writers: a selection of sketches from contemporary authors, Volume 4, Gale Research, 1991. ISBN 0-8103-7915-5, ISBN 978-0-8103-7915-2
  2. Janet G. Vaillant. Black, French, and African: a life of Léopold Sédar Senghor, Harvard University Press, 1990. ISBN 0-674-07623-0, ISBN 978-0-674-07623-5