Tofauti kati ya marekesbisho "Fonolojia"

316 bytes added ,  miaka 3 iliyopita
no edit summary
Jambo lingine la kuzingatia ni vipashio vya kiuchambuzi vya matawi haya mawili. Wakati fonetiki kipashio chake cha msingi ni "foni", fonolojia kipashio chake cha msingi ni "fonimu". Kwa kuzingatia maelezo ya hapo awali, ni wazi kuwa foni ni nyingi zaidi kuliko fonimu, kwa kuwa foni ni kila sauti itamkwayo na binadamu, wakati fonimu ni sauti zile tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha mahususi. Hivyo, kuna fonimu za Kiswahili, za Kiingereza, za [[Kichina]], n.k., lakini foni si za lugha yoyote, wala huwezi kusema kwa uhakika kuna foni ngapi, kwa kuwa bado kuna lugha nyingi [[duniani]] ambazo hazijatafitiwa.
[[Historia]] ya fonolojia inaweza kuwa imeanza na [[Ashtadhyayi]], [[sarufi]] ya [[Kisanskrit]] iliyoandikwa na [[Pāṇini]] katika [[karne ya 4 KK]]. Kwa namna ya pekee [[Shiva Sutras]], nyongeza ya Ashtadhyayi, inaorodhesha fonemi ya lugha hiyo, pamoja na kujadili [[mofolojia]], [[sintaksia]] na [[semantiki]].
 
== Marejeo ==
*[[TUKI]] 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", [[Chuo Kikuu cha Dar es Salaam]]