Mdudu mabawa-manyoya : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mbegu na pendekezo jina
Sahihisho
Mstari 9:
| nusufaila = [[Hexapoda]] (Wanyama wenye miguu sita)
| ngeli = [[Insecta]] (Wadudu)
| ngeli_ya_chininusungeli = [[Pterygota]] (Wadudu wenye mabawa)
| oda = [[Trichoptera]] (Wadudu wenye mabawa yanayobeba manyoya)
| subdivision = '''Nusuoda 2 na familia za juu 10''':
Mstari 25:
** †Vitimotaulioidea
}}
'''Wadudu mabawa-manyoya''' ni [[wadudu]] wadogo hadi wakubwa kiasi wa [[oda]] [[Trichoptera]] (trichos = [[nyoya]], ptera = [[bawa|mabawa]]) katika [[nusungeli]] [[Pterygota]] (wenye mabawa). Jina lao ni tafsiri ya jina la kisayansi. Wadudu hawa wanafanana na [[nondo]] wadogo (oda [[Lepidoptera]]) na oda hizi zina mnasaba. Lakini badala ya [[gamba|vigamba]] vya [[bawa|mabawa]] ya Lepidoptera mabawa ya Trichoptera yanabeba manyoya.
 
[[Lava]] wa [[spishi]] nyingi huishi majini lakini wale wa [[familia (biolojia)|familia]] [[Limnephilidae]] huishi kwenye ardhi. Wanatoa [[hariri]] ili kuitengenezea utando au kipeto. Wanaotengeneza utando huishi katika maji yanayotiririka. Utando ni kimbilio na inafaa kutega chakula ([[mnyama|wanyama]] wadogo, [[algae|viani]], masalio). Kipeto cha lava wengine ([[mdudu-kipeto|wadudu-kipeto]]) kinatumikia kwa kukinga kiwiliwili chororo dhidi ya adui na kinashirikisha vitu vigumu kama chembe za mchanga, vijiti, koa n.k. Lava anaweza kutoa kichwa na kidari (toraksi) na kutembea akivuta kipeto. Kuna lava ambao huishi majini bila utando au kipeto. Hawa hutumia hariri tu ili kutengeneza kifukofuko cha [[bundo]].