Kivunjajungu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mbegu
Maana ya jina la kisayansi
Mstari 34:
}}
[[File:MantisLegGBMNH.jpg|thumb|250px|Mabadiliko ya mguu wa mbele: koksa ni ndefu sana na inafanana na femuri. Femuri binafsi ni kiungo cha kwanza cha sehemu ya kukamata ya mguu.]]
'''Vivunjajungu''', '''vunjajungu''' au '''katamasikio''' ni [[wadudu]] wadogo hadi wakubwa kiasi wa [[oda]] [[Mantodea]] (mantis = nabii, eidos = umbo) katika [[nusungeli]] [[Pterygota]] (wenye [[bawa|mabawa]]). Wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki na kusini (au kaskazini) kwa kanda za wastani. Kiwiliwili chao ni kirefu na chembamba. [[Mguu|Miguu]] ya mbele imetoholewa kwa kukamata [[arithropodi]] wengine na hata [[vertebrata]] wadogo. Kwa kawaida [[koksa]] ([[w:coxa|coxa]]) za miguu ya wadudu ni fupi, lakini zile za miguu ya mbele ya vivunjajungu zimerefuka. [[Femuri]] na [[tibia]] zina [[mwiba|miiba]] na [[jino|meno]] inayowezesha mdudu kushika vizuri mawindo yake. Kama takriban wadudu wote vivunjajungu wana [[toraksi]] yenye sehemu tatu, lakini ile ya mbele, [[protoraksi]], ni ndefu kuliko mbili nyingine pamoja na imeungwa vinamo na [[mesotoraksi]]. Hii inawezesha mdudu asogeze [[kichwa]] na miguu ya mbele pande zote wakati kiwiliwili kinatulia. Hata [[shingo]] ni kinamo na spishi kadhaa zinaweza kuzungusha kichwa kwa nyuzi 180.
 
==Picha==