Tofauti kati ya marekesbisho "Wambunga"

13 bytes added ,  miaka 4 iliyopita
Baada ya kutoelewana miongoni mwa makundi ya Wangoni kukapelekea [[chuki]] iliyosababisha viongozi wa makundi hayo kuuana wenyewe kwa wenyewe. Hivyo Mputa akauawa, na [[Mwana|mwanae]] Malunda akawa [[mtawala]] wa kundi hilo. Baadaye Malunda akawa na wasiwasi wa maisha yake kutokana na hali hiyo, hivyo akaamua kurudi na kundi la Wangoni maseko katika [[Zimbabwe]] ya leo walikotokea awali.
 
Lakini katika hilo baadhi yao waligoma kurudi Zimbabwe, ndipo baada ya Malunda kuondoka waliobaki wakahama pale Songea na kusogea [[mlima Mbunga]] ulioko pembezoni mwa [[mkoa wa Ruvuma]]. Baadaye, walipoona makundi ya Wangoni wakiendelea kupigana wao kwa wao, wakaamua kuondoka hapo [[mlima]] Mbunga na kuambaambaa [[Wilaya ya Ulanga|UlangaKilombero (Ifakara)]] (leo katika [[mkoa wa Morogoro]]), hasa kwenye [[bonde]] la [[mto Kilombero]].
 
Walijulikana kwa [[matamshi]] yao kuwa Wangoni, lakini wao walijiita Wambunga kwani wametokea mlima Mbunga. Hiyo ilitokana na kuchoshwa na vita, maana wote waliwatambua Wangoni kwa kupenda vita, kumbe kwa kusema hivyo wangebaki salama wenyeji wao wasiwadhuru, maana wakati huo Wangoni walishaanza uchokozi wa kivita na [[Muyugumba]], kiongozi wa Wahehe.
Anonymous user