Mlima : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 20:
Milima huwa na historia inayoweza kutazamiwa kama maisha ya mlima. Milima hutokea kutokana na miendo ndani ya [[ganda la dunia]].
 
[[Mabamba ya gandunia]] husukumana na kusababisha kukunja kwa sehemu fulani. [[Milima kunjamano]] kama [[Himalaya]] katika [[Asia]], [[Alpi]] za [[Ulaya]] au [[Atlas]] ya [[Afrika ya Kaskazini]] ilitokea hivyo. Miendo ya [[gandunia]] husababisha pia kutokea kwa milima baharini inayoweza kutokea juu ya uso wa maji kama [[visiwa]]. Milima iliyotokea kutokana na kukunjwa mara nyingi huonekana kama safu ndefu ya milima.
 
Njia nyingine ya kutokea kwa milima ni [[volkeno]]. Hapa [[magma]] (mwamba moto ulioyeyuka) inapanda kutoka [[koti ya dunia]] inakuta njia kupitia nafasi katika ganda la dunia na kufika usoni kwa umbo la [[zaha (lava)]]. Hapa zaha inaganda kuwa [[mwamba]] imara. Kama akiba ya magma chini ya volkeno ni kubwa inaendelea kupanda juu na kutoka kwenye kasoko ya volkeno. Inapanda juu ya zaha iliyoganda tayari na kwa njia hii volkeno inazidi kukua.