Uislamu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 55:
Nguzo hizo ziliwekwa taratibu katika mwaka ulioonyeshwa katika mabano: shahada (610), sala tano (622), zaka (623), saumu (623), hija (628).
 
# ''[[Shahada]]'': (Kiarabu: الشهادة) Nguzo ya kwanza katika Uislamu hujumuisha kutoa kauli mbili: ''Hakuna Mola apasaye Kuabudiwa ila Allah na Muhammad ni Mtume wake''. Kauli hizo hutolewa pale mwanadamu anapoingia Uislamu.
# '' [[Salat]]'': (kwa [[Kiarabu]]: صلاة‎) ni [[sala]] inayofuata utaratibu maalumu mara tano kila siku: Asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Kabla ya kuingia katika ibada hii Mwislamu anapaswa kufanya [[wudhu]] ambayo ni tendo la kutakasa mwili kwa maji au -kama hakuna- kwa kutumia vumbi badala yake. Salat ina maneno yake na pia namna ya kusimama au kujinama. Salat hii ni tofauti na [[dua]] (دعاء) au sala ya kuomba kwa hiari.
# ''[[Zakat]]'': (Kiarabu: زكاة‎‎) Nguzo ya tatu ya Uislamu nayo ni ibada inayomuelekeza Mwislamu kuwaangalia Waislamu wenzake kwa hali na mali, na kushughulikia mahitaji yao ya maisha, kwa kutoa fungu la mali yake asilimia 2.5 kila mwaka kwa mwenye uwezo na kuwapa wale walio maskini na wasiojiweza ili nao waweze kuishi vizuri.
# Funga/[[Swaum]]: (Kiarabu: صوم) Wakati wa mwezi [[Ramadani]] kila Mwislamu anapaswa kufunga chakula na kinywaji chote kuanzia asubuhi hadi jioni. Watoto na wagonjwa hawapaswi kutekeleza wajibu huu. Waislamu wanaona maana ya ibada hii kumkurubisha Mwislamu na Mola wake na kumfanya amche na kumuogopa zaidi, kwani saumu humsaidia Mwislamu kufahamu shida na taabu ambazo wale wasiokuwa na uwezo wanazipata wakiwa na njaa na hawana cha kukila, na kwa hivyo, huingiwa na huruma na kuwa na moyo wa kutaka kuwasaidia na kuwaondoshea shida hizo.
# ''[[Hajj]]'' (Kar. الحجّ ''alhajj''): Kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kwenda hijja [[Maka]] mara moja katika maisha yake wakati wa mwezi Dhul-Hija. Nguzo hii inawapa fursa Waislamu ulimwenguni kukutana na wenzao na kujua hali zao na kupata nafasi ya kuomba maghfira na msamaha kwa madhambi yao katika mkutano mkubwa kabisa wa wanadamu ulimwenguni.