Yohane wa Nepomuk : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|220px|Mt. Yohane wa Nepomuk. File:Czechowicz St. John Nepomuk.jpg|thumb|right|''Kifodini cha Mt. Yohan...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:14, 21 Februari 2017

Yohane wa Nepomuk (kwa Kicheki: Jan Nepomucký; kwa Kijerumani: Johannes Nepomuk; kwa Kilatini: Ioannes Nepomucenus[1]) Nepomuk, 1345 hivi – Prague, 20 Machi 1393)[2] alikuwa padri wa Bohemia (leo nchini Ucheki). Aliuawa kwa kutoswa mtoni Vltava kutoka darajani kwa agizo la mfalme Wenseslaus, mfalme wa Warumi na wa Bohemia.

Mt. Yohane wa Nepomuk.
Kifodini cha Mt. Yohane wa Nepomuk kilivyochorwa na Szymon Czechowicz, National Museum in Warsaw, Polandi.

Baadaye ilisimuliwa kwamba alikuwa muungamishi wa malkia na kwamba alikataa ombi la mfalme la kutoboa siri za kitubio. Kwa msingi huo anahesabiwa kama mfiadini wa kwanza wa siri ya kitubio na msimamizi dhidi ya masingizio.[2]

Alitangazwa mwenye heri tarehe 31 Mei 1721, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 19 Machi 1729.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 20 Machi.

Tanbihi

  1. Sanctus Johannes Nepomucenus Christi Heiliger Blut-Zeug. 1723. 
  2. 2.0 2.1 Krčmář, Mgr. Luděk. "Saint John of Nepomuk". SJN.cz. If in 1369 John of Pomuk was a notary public, he must have been more than twenty years old. Thus he was probably born sometimes between 1340 and 1350 [1349]. 

Viungo vya nje

 
WikiMedia Commons
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.