Chuo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
'''Chuo''' ni taasisi ya [[elimu]] ya pekee. Inatoa mafunzimafunzo ya [[kazi]] fulani. Mifano ni chuo cha [[ufundi]], chuo cha [[kilimo]] au chuo cha [[ualimu]]. Kwa kila namna chuo kinaanza kufundisha watu baada ya kumaliza ngazi fulani ya [[shule]].
 
==Asili na maana ya neno "chuo"==
Kiasili maana ya [[neno]] "chuo" kilikuwailikuwa sawa na "kitabu". Kwa maana hii chuohiyo linatumiwa kwa mfano katika [[tafsiri]] za [[Biblia]] kama vile [[Injili]] [[Lk|ya Luka]] 4:17 "Yesu akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo".<ref>[http://www.biblepage.net/sw/kuchagua-kitabu/luka-4.php?chxverse=17 Luka 4:17] hii ni toleo la "Union version" (1952) linalofuata hapa tafsiri ya [[Edward Steere]] ya 1883; tafsiri za kisasa hutumia hapa "kitabu" badala ya "chuo". Tafsiri ya "[http://quranitukufu.net Qurani Tukufu]" ya Sheikh Ali Muhsin Al Barwani inatumia kote neno "kitabu", si "chuo".</ref>

Kutokana na maana hii asilia "chuo" kimekuwa pia neno la kutaja mahali pa kujifunza kusoma, kwa hiyo katika [[Kiswahili]] cha miaka iliyopita kiliweza kutaja pia [[shule]].<ref>A. C. Madan Swahili-English Dictionary Oxford 1903: "Chuo, n. {vy-), (i) book; (2) school" ([https://ia801409.us.archive.org/2/items/swahilienglishdi00madauoft/swahilienglishdi00madauoft.pdf online hapa])</ref>.

Leo hii matumizi ya neno limebadilikayamebadilika, kwa maana ya "kitabu" huptikanahupatikana tu katika matini zenye Kiswahili cha zamani na kama mahali au taasisi ya elimu kwa jumla, neno "[[shule]], skuli"<ref>"Shule" kutoka [[jer.Kijerumani]] ''Schule'', "skuli" kutoka ing.[[Kiingereza]] ''school''</ref> limechukua nafasi pana zaidi.
 
==Viwango vya vyuo==
Jina la "Chuo" linaweza kutaja taasisi zinazotoa elimu kwa ngazi tofauti sana. Hii itategemea na muundo wa elimu katika nchi mbalimbali.
*Chuo cha ufundi stadi, kwa mfano [[useremala]], mara nyingi kitafundisha [[wanafunzi]] waliotoka kwenye [[shule ya msingi]] na kuwafundisha ufundi fulani kama useremala, yaani matumizi ya vifaa vya fani hii na kuwawezesha kujengakutengeneza [[fenicha]] au kushughulikia kazi zinazohusu matumizi ya [[ubao]] katika [[ujenzi wa majengo ]].<ref>Kwa jumla linganisha tovuti ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) http://www.veta.go.tz/index.php/sw</ref>
* Chuo cha [[uganga]] kinapokea watu waliomaliza [[Sekondari|shule ya sekondari]] na kuwapa elimu wa kuwa msaidizi wa [[mwuguzi]] au [[daktari]] aliyesoma [[tiba]] kwenye [[chuo kikuu]] ("medical assistant").
*Vyuo vingine vinaweza kuwapeleka wanafunzi wao hatahadi ngazi ya [[diploma]] au hata hadi [[bachelor]].
*Katika nchi kadhaa chuo kinatoa [[elimu ya juu]] lakini katika fani moja tu, tofauti na [[chuo kikuu]] kinachofundisha fani mbalimbali na pia kuweka uzito kwenye [[uchunguzi]] wa kitaalamu, si mafundisho pekee..
 
==Wanafunzi na walimu==