Alfabeti ya Kigiriki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
upungufu
Mstari 14:
 
== Matumizi ya namba ==
Kila herufi ilikuwa pia na matumizi kama [[tarakimu]] ya [[namba]] kwa sababu Wagiriki wa Kale hawakuwa na alama za pekee za namba. Herufi [[tatu]] za kihistoria ambazo hazikutumiwa tena kwa maandishi ziliendelea kama alama za namba, yaani Digamma au Stigma = 6 (alama ϝ au ς), Koppa = 90 (alama ϙ au ϟ) na Sampi = 900 (alama ͳ au ϡ au kama kwenye sanduku).
 
Kwa kutofautisha herufi na namba alama yake ilipewa mstari mdogo juu yake kama αʹ = 1, βʹ = 2, γʹ = 3. Kwa namba kuanzia 1,000 mstari upande wa kushoto uliongezwa, kwa mfano ͵α = 1,000, ͵β = 2000, ͵βηʹ = 2008.