Kalenga : Tofauti kati ya masahihisho

1,429 bytes added ,  miaka 6 iliyopita
no edit summary
No edit summary
No edit summary
'''Kalenga ''' ni jina la kata ya [[Wilaya ya Iringa Vijijini]] katika [[Mkoa wa Iringa]], [[Tanzania]]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,963 waishio humo.<ref>[http://www.wavuti.weebly.com/uploads/3/0/7/6/3076464/census20general20report20-202920march202013_combined_final20for20printing1.pdf Sensa ya 2012, Iringa Region- Iringa District Council]</ref> Msimbo wa posta ni 51201.
==MakumbushoKalenga na historia ya mtemi Mkwawa==
[[Picha:Skull of Mkwawa.jpg|thumb|320px|Fuvu la Mtemi Mkwawa katika makumbusho ya Kalenga]]
Hapa Kalenga kuna makumbusho kwa heshima ya Mtemi [[Mkwawa]] aliyeongoza upinzani wa [[Wahehe]] dhidi ya [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani|ukoloni wa Kijerumani]] katika miaka ya 1891 - 1896. Fuvu la Mkwawa lililowahi kupelekwa Ujerumani inasemekana kuhifadhiwa hapa tangu kurudishwa 1956.
Kalenga ilikuwa makao makuu ya ya Mtemi [[Mkwawa]]<ref>[http://www.mkwawa.com/kalenga Fungu "Kalenga" kwenye Mkwawa.com], iliangaliwa Machi 2017</ref> aliyeongoza upinzani wa [[Wahehe]] dhidi ya [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani|ukoloni wa Kijerumani]] katika miaka ya 1891 - 1896. Mkwawa aliwahi kujenga boma imara ya mawe baada ya kujifunza kuhusu uenezaji wa Wajerumani kutoka sehemu za pwani. Boma hii liliitwa Lipuli. Ujenzi ulianza mnamo 1887 ukachukua miaka minne.
 
Baada ya kushindwa kwa jeshi la [[Schutztruppe]] la Kijerumani katika mapigano ya [[Lugalo]] mwaka 1891 Wajerumani walirudi kwa nguvu zaidi wakashambulia Lipuli - Kalenga kwenye Oktoba 1894 kwa silaha kali kama [[mizinga]] na [[bombomu]]. Mkwawa alifaulu kukimbia wakati wa kutekwa kwa boma. Akaendelea kuendesha [[vita ya msituni]] hadi kujiua mwaka 1898 alipoona hatari ya kukamatwa ilhali alijeruhiwa vibaya. Inasemekana Wajerumani walikata kichwa chake na kutuma fuvu Ujerumani.
 
Baada ya kushindwa kwa Ujerumani katika [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]] washindi hasa Uingereza walisisitiza fuvu lirudishwe na hivyo kuna fungu 246 katika [[Mkataba wa Versailles]] linalotaja fuvu la Mkwawa. Wajerumani walidai baadaye wanashindwa kulikuta na hivyo ilichelewa hadi baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia wakati jeshi la Uingereza lilikuwa na utawala juu ya sehemu za Ujerumani ya kwamba Waingereza waliteua fuvu moja katika mkusanyiko wa Makumbusho wa Bremen na kulituma Tanganyika kama fuvu la Mkwawa.
Hapa Kalenga kuna makumbusho kwa heshima ya Mtemi Mkwawa na fuvu lake linahifadhiwa hapa tangu kurudishwa 1954.
 
==Marejeo==
{{marejeo}}
 
{{Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini}}