Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
→Vita katika nchi mbalimbali: Nimerekebisha sarufi Tags: Mobile edit Mobile app edit |
|||
Mstari 46:
* [[Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani]] ilivamiwa na Afrika Kusini na [[jeshi la ulinzi la Kijerumani]] likajisalimisha mnamo Julai 1915.
* [[Kamerun]] ilivamiwa na Ufaransa na Uingereza kutoka makoloni yao ya [[Nigeria]] na [[Afrika ya Kati ya Kifaransa]]. Jeshi la ulinzi likajisalimisha katika Februari [[1916]].
* [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]] ilikuwa mahali pa mapigano yaliyoendelea kwa miaka yote ya vita. Jeshi la Ulinzi wa Kijerumani lililoitwa [[Schutztruppe]] chini ya uongozi wa [[Paul von Lettow-Vorbeck]] lilifaulu kutetea eneo la koloni dhidi ya mashambulio ya kwanza ya Waingereza kutoka [[Kenya]] hadi 1916. Kwenye Novemba 1914 jeshi la [[askari]] 8,000 kutoka [[Uhindi]] lilishindwa kwenye [[mapigano ya Tanga]]. Hadi mwanzo wa 1916 Waingereza walikusanya jeshi kubwa kutoka Afrika Kusini na Uhindi wakafaulu kutwaa sehemu kubwa ya koloni hadi Agosti 1916. Jeshi la ulinzi likaendelea kushika sehemu ya kusini ya koloni hadi [[1917]] ilipopaswa kuhamia eneo la [[Ureno|Kireno]] katika [[Msumbiji]]. Waingereza na Wareno walishindwa kulishika kundi la Kijerumani. Mwaka 1918 Lettow-Vorbeck alirudi [[Tanganyika]] akaingia [[Rhodesia ya Kaskazini]] alipoambiwa na Waingereza mnamo Novemba 1918 ya kwamba vita ya Ulaya ilikwisha tayari.
== Mwisho wa vita ==
|