Jua : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Masahihisho aliyefanya 188.64.240.39 (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Riccardo Riccioni
No edit summary
Mstari 2:
'''Jua''' ni [[nyota]] ambayo ni karibu na [[dunia]] yetu kuliko nyota nyingine. Jua ni [[kitovu]] cha [[mfumo wa jua]] likizungukwa na [[sayari]] nane. [[Dunia]] yetu ni moja ya sayari hizo katika [[mfumo wa jua na sayari zake]].
 
==Umbo la jua==
[[Umbo]] la jua linakaribia [[tufe]] kamili. [[Maada]] yake ni [[Utegili (fisikia)|utegili]] yaani [[gesi]] ya [[joto]] sana inayoshikwa na [[nguvu]] ya ki[[sumaku]].
 
Line 8 ⟶ 9:
Ki[[kemia]] masi ya jua ni hasa [[hidrojeni]] (73%) na [[heli]] (25%). Kiasi kinachobaki ni [[elementi]] nzito zaidi, kama vile [[oksijeni]], [[kaboni]], [[chuma]] na [[nyingine]]. Hata kama hizi elementi nzito ni [[asilimia]] ndogo tu za masi ya jua, bado zinalingana na mara 5,000 masi ya dunia kutokana na ukubwa wa jua.
 
==Historia ya jua==
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa jua liliundwa takriban miaka [[bilioni]] 4.57 iliyopita kutoka katika [[gimba]] kubwa la ma[[wingu]] lililoundwa na asilimia kubwa za hidrojeni.
 
==Mnururisho na upepo wa jua==
Jua linatoa [[mwanga]], [[joto]] na [[mnururisho]] mwingine wa aina mbalimbali. Sehemu ya mnururisho huu unatoka kwa umbo la vyembe kama protoni na elektroni ambazo kwa jumla hujulikana pia kama [[upepo wa jua]]. Masi ya upepo wa jua ni takriban tani moja kwa kila sekunde.<ref>Carroll, Bradley W.; Ostlie, Dale A. (1995). An Introduction to Modern Astrophysics (revised 2nd ed.). Benjamin Cummings. p. 409. ISBN 0-201-54730-9.</ref> [[Asili]] ya [[nishati]] hii ni mchakato wa [[myeyungano wa kinyuklia]] ndani yake. Katika myeyungano huo hidrojeni inabadilishwa kuwa heli. Elementi nyingine zinatokea pia kwa kiasi kidogo. Badiliko kutoka hidrojeni kwenda heli inaachisha nishati inayotoka kwenye jua kwa njia ya mnururisho.
 
[[Nishati]] ya mnururisho huu ni msingi wa maisha ya [[mmea|mimea]] na [[kiumbehai|viumbe hai]] katika dunia. Nuru ya jua inabadilishwa na mimea kwa njia ya [[usanisinuru]] kuwa [[nishati ya kikemia]] inayojenga [[miili]] yao itakayokuwa [[lishe]] tena ya mimea na wanyama.
 
==Tanbihi==
<references/>
 
==Viungo vya Nje==
 
 
{{mbegu-sayansi}}