Burundi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 124:
Katika Burundi kikosi cha kwanza cha Kijerumani kilifika mnamo [[1896]] wakakuta ufalme wa mwami wakaridhika kumwacha mwakilishi mkazi (resident) katika [[mji mkuu]] [[Gitega]] ambaye hakuhusika na mambo ya utawala wa ndani. Wakati ule eneo lilijulikana kwa jina "[[Urundi]]". Hapa sawa na Rwanda na [[Bukoba]] Wajerumani walitumia [[mbinu]] ya [[eneo lindwa]] ingawa walikuwa pia na majadiliano kuingiza falme hizi za kienyeji moja kwa moja ndani ya koloni lao.
 
Baada ya [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]] Burundi pamoja na Rwanda ilikabidhiwa kwa [[Ubelgiji]] kwa niaba ya [[Shirikisho la Mataifa]] kama [[eneo la kudhaminiwa]] lililoitwa Ruanda-Urundi. Kimsingi Wabelgiji waliendelea na mfumo wa Wajerumani uliomwachia mtemi [[mamlaka]] kubwa. Waliweka Ruanda-Urundi chini ya serikali ya Kongo ya Kibelgiji.
 
Lakini baadaye walianza kuingilia zaidi, na ilhali wakati ule walipendelea Watutsi, karibu na machifu wote walikuwa Watutsi, na Wahutu walipotea katika nafasi za uongozi kimahali.
 
Tangu mwaka 1946 Shirikisho la Mataifa lilikwisha na Ubelgiji ilipokea wito wa kutawala Ruanda-Urundi na [[Umoja wa Mataifa]].
[[Picha:BujumburaFromCathedral.jpg|300px|thumbnail|Jiji la Bujumbura]]