Albano wa Uingereza

Albano wa Verulamium (Uingereza Kusini Mashariki) anahesabiwa kuwa Mkristo mfiadini wa kwanza kutoka Britania ya Kirumi.

Mt. Albano.

Alikuwa bado Mpagani alipomficha padri fulani nyumbani mwake. Baada ya huyo kumfundisha imani ya Kikristo, alibadilishana naye mavazi akajitokeza kukamatwa badala yake. Hapo aliteswa kikatili akakatwa kichwa[1].

Makadirio ya mwaka wa kifodini chake yanatofautiana sana: 209, 251 hivi na hata 304.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 22 Juni[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Niblett, Rosalind (2001). Verulamium: The Roman City of St Albans. Tempus Publishing Ltd. ISBN 0-7524-1915-3. 

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.