Alvaro Morata

Mchezaji wa soka wa Hispania

Álvaro Borja Morata Martín (kwa matamshi ya Kihispania: [alβaɾo moɾata]; alizaliwa 23 Oktoba 1992) ni mchezaji wa soka wa Hispania ambaye anacheza kama mshambuliaji wa Atletico Madrid kwa mkopo kutoka kwa Klabu ya Uingereza na timu ya taifa ya Hispania.

Alvaro Morata
binadamu
Jinsiamume Hariri
Nchi ya uraiaHispania Hariri
Nchi anayoitumikiaHispania Hariri
Jina katika lugha mamaÁlvaro Morata Hariri
Jina la kuzaliwaÁlvaro Borja Morata Martín Hariri
Jina halisiÁlvaro Hariri
Jina la familiaMorata Hariri
Tarehe ya Kuzaliwa23 Oktoba 1992 Hariri
Mahali alipozaliwaMadrid Hariri
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihiKihispania Hariri
Kaziassociation football player Hariri
Nafasi anayocheza kwenye timuforward Hariri
MchezoMpira wa miguu Hariri
Namba ya Mchezaji19 Hariri
AmeshirikiUEFA Euro 2016 Hariri
LigiLaLiga Hariri
Alvaro Morata Juventus
Alvaro Morata akiwa Juventus
Alvaro Morata.
Alvaro Morata.

Kazi ya klabu hariri

Real Madrid hariri

Alianza kazi yake katika klabu ya Real Madrid, akicheza kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2010 na kuonekana katika michezo 52 rasmi madoli11, hasa kushinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2014.[onesha uthibitisho]

Juventus hariri

Baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2014, alihamia Juventus kwa euro milioni 20 mwaka 2014, kushinda mara mbili ndani ya Serie A na Coppa Italia katika msimu wake wote kabla ya kununuliwa na Real madrid kwa mara nyingine kwa 30,000,000.

Kurudi Real Madrid hariri

Mnamo tarehe 21 Juni 2016, Real Madrid ilimrejesha tena Morata kutoka katika klabu ya Juventus kwa € 30,000,000.Mechi yake ya kwanza ya ushindani ilikuwa mnamo tarehe 9 Agosti, na kushinda 3-2 dhidi ya Sevilla katika Kombe la Super Cup UEFA, na kubadilishana na Benzema baada ya dakika 62.G oli lake la kwanza alilipata katika mechi waliyoshinda 2-1 dhidi ya Celta Vigo mnamo Agosti 27.

Alishinda La Liga na Ligi ya Mabingwa mnamo mwaka 2016-17 kabla ya kujiunga na Chelsea mnamo mwaka 2017 kwa ada ya rekodi ya klabu ya karibu milioni 60. Mnamo Januari 2019, alihamia Atlético Madrid kwa mkopo na angejiunga na kilabu kabisa tarehe 1 Julai 2020.

Chelsea hariri

Mnamo tarehe 19 Julai 2017, Chelsea walitangaza kuwa wamekubaliana na Real Madrid kwa uhamisho wa Morata, kwa ada ya rekodi ya klabu ya £ 60 milioni. Mnamo tarehe 21 Julai, alifanikiwa kupitisha matibabu yake na rasmi akawa mchezaji wa klabu ya Chelsea.

Mnamo tarehe 5 Novemba 2017, Morata alifunga goli katika mechi ambayo walikuwa nyumbani dhidi ya Manchester United kwa goli1-0. Na katika mechi nyinine ambayo Chelsea walishinda 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika uwanja wa nyumbani Stamford Bridge.

Msimu wa 2018-19 hariri

Mnamo 18 Agosti 2018, akifunga goli la pili katika ushindi wa nyumbani wa 3-2 dhidi ya Arsenal,Na pia Oktoba 4, alifunga goli katika ushindi wa 1-0 dhidi ya MOL Vidi katika hatua ya makundi katika UEFA Europa League.Mwezi mmoja baadaye, alifunga magoli mawili kusaidia kupata ushindi dhidi ya Crystal Palace kwa magoli 3-1 katika mechi ya ligi.

Atletico Madrid hariri

Mnamo tarehe 27 Januari 2019, Morata alirudi hispania katika klabu ya Atletico Madrid akijiunga na klabu kwa mkataba wa mkopo wa miezi 18.Alicheza katika ligi hiyo kwa mara ya kwanza mnamo Februari 3, katika mechi waliyokupoteza kwa kufungwa 0-1 mbali dhidi ya Real Betis.Alifunga goli lake la kwanza tarehe 24 Februari, katika ushindi wa nyumbani wa magoli 2-0 dhidi ya Villarreal.  

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alvaro Morata kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.