Antonina wa Nisea (Nisea, Bitinia, leo nchini Uturuki, karne ya 3 - Nisea, 303 hivi) alikuwa mwanamke Mkristo ambaye kwa ajili ya imani yake hiyo alifungwa miaka miwili, aliteswa kikatili na kuning'inizwa siku tatu na hatimaye alichomwa moto kwa amri ya gavana Prisiliani wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian[1].

Picha takatifu ya Mt. Antonina.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Mei[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.