Augustino Webster, O.Cart. (alifariki Tyburn, 4 Mei 1535) alikuwa padri wa Uingereza, priori wa monasteri ya Wakartusi ya Epworth[1][2].

Mt. Augustino Webster.

Kwa kukiri imani ya mababu na kwa kukataa kiapo cha kumtii mfalme Henri VIII kama mkuu wa Kanisa Uingereza badala ya Papa[3][4] alinyongwa ila kabla hajafa alikatwa vipandevipande ambayo vilitundikwa sehemu mbalimbali za mji. Pamoja naye waliuawa mapriori wawili wengine wa shirika hilo, Yohane Houghton na Robati Lawrence, tena padri Richard Reynolds wa shirika la Mt. Birgita na paroko mwanajimbo Yohane Haile.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 9 Desemba 1886 na mtakatifu tarehe 25 Oktoba 1970 na Papa Paulo VI.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe ya kifodini chake[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.