Augusto wa Caserta

Augusto wa Caserta (alifariki 490 hivi) alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo wa Italia Kusini lakini alikuwa mzaliwa wa Afrika Kaskazini.

Baada ya kuteswa na Wavandali Waario kwa sababu ya imani yake, alifukuzwa akiwa na wenzake 12, inasemekana kwa kuachwa baharini katika meli mbovu isiyoweza kuendeshwa.

Labda wakati huo alikuwa padri au askofu tayari. Baada ya kufika Italia, aliongoza jimbo la Caserta.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.