Babu kwa mjukuu wake ni hasa baba wa mzazi wake mmojawapo. Katika DNA anachangia 25%.

Kipenzi - Babu na mjukuu, mchoro wa Georgios Jakobides (1890)

Inakadiriwa kwamba miaka 30,000 iliyopita idadi ya watu waliofikia umri wa kuona wajukuu wao iliongezeka sana na kuwezesha ushirikishaji wa ujuzi na mang'amuzi mbalimbali kuliko awali.[1][2]

Pia babu anaweza kushika nafasi ya baba ikiwa huyo hayupo (k.mf. amekufa) na kumfaidisha mtoto kimalezi. Hata kama baba yupo, babu anaweza kutoa mchango mzuri katika makuzi ya mtoto.

Tanbihi hariri

  1. Wong, Kate. The Mysterious Downfall of the Neandertals. Scientific American. Iliwekwa mnamo 2013-03-24.
  2. Caspari, R. (2012). "The Evolution of Grandparents". Scientific American 22: 38. doi:10.1038/scientificamericanhuman1112-38. 

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: