Bahari ya Java ni sehemu ya bahari iliyopo kati ya visiwa vya Indonesia vya Borneo upande wa kaskazini, Java upande wa kusini, Sumatra upande wa magharibi, na Sulawesi upande wa mashariki.

Ramani ya Bahari ya Java.
Pwani ya Bahari ya Java karibu na Anyer

Mlangobahari wa Karimata upo kwenye kaskazini magharibi na kuiunganisha na Bahari ya Kusini ya China.

Eneo lake ni la km² 320,000.

Uvuvi ni shughuli muhimu ya kiuchumi katika Bahari ya Java. Kuna zaidi ya spishi 3,000 za viumbe vya baharini katika eneo hilo. Kuna pia hifadhi kadhaa za kitaifa kama Karimunjawa.

Eneo linalozunguka Bahari ya Java ni shabaha maarufu ya utalii. Wengi wanakuja kupiga mbizi na kupata picha za viumbe chini ya maji, mabaki ya meli zilizozama, matumbawe na sifongo.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia yalitokea hapa mapigano ya baharini katika miezi ya Februari na Machi ya mwaka 1942 ambapo jeshi la majini la Japani lilishinda mataifa ya ushirikiano Uholanzi, Ufalme wa Muungano, Australia na Marekani yaliyojaribu kutetea Java.

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

5°S 110°E / 5°S 110°E / -5; 110