Bahari ya Liguria ni sehemu ya Bahari Mediteranea iliyoko upande wa magharibi wa rasi ya Italia.

Ramani ya Bahari ya Liguria

Umbo lake ni kama pembetatu kuanzia mpaka wa Italia na Ufaransa, hadi rasi ya kaskazini ya kisiwa cha Korsika na tena hadi rasi ya San Pietro (44°03′N 9°50′E / 44.050°N 9.833°E / 44.050; 9.833) karibu na mji wa La Spezia, Italia.[1]

Bahari hii inapokea maji ya mto Arno pamoja na mito mingine inayotelemka kutoka milima ya Apenini.

Bandari muhimu zaidi ni Genova, La Spezia na Livorno.

Kina kirefu cha kufikia mita 2,850 kinapatikana karibu na Korsika.

Picha hariri

Marejeo hariri

  1. Limits of Oceans and Seas, 3rd edition. International Hydrographic Organization (1953). Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-10-08. Iliwekwa mnamo 7 February 2010.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: