Bandari ya Bagamoyo

Bandari ya Bagamoyo ilipangwa kujengwa huko Bagamoyo, nchini Tanzania. Ilipangwa kuwa moja ya miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ya serikali nchini humo. Bandari ya Bagamoyo na eneo lake la ushirika linalojengwa kushughulikia msongamano katika bandari ya zamani na kusaidia Tanzania kuwa kituo cha kuongoza kwa usafirishaji Afrika Mashariki.[1]

Bandari ya Bagamoyo

Mikataba ya kuanza ujenzi wa bandari hii ilisainiwa mnamo Oktoba mwaka 2015 na iliwekwa wazi kukamilika awamu ya I ya mradi wa ujenzi mnamo mwaka 2017.[2] Mradi huo ulifutwa na serikali mpya miezi 3 baadaye mnamo Januari mwaka 2016. [3][4]

Mnamo mwaka 2018, mradi uliendelea, na kazi ilianza katikati ya mwaka huo. Bandari ilitakiwa kujengwa kwa kushirikiana na serikali na Bandari ya Wauzaji wa China, na kujumuisha eneo maalum la kiuchumi. Mradi huo ulitarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani bilioni 10 na kuungwa mkqono na Oman.[5][6][7]

Ghafla mradi ulisimamishwa. Inasemekana ni kwa sababu ya Rais John Pombe Magufuli kutaka kuelekeza nguvu zake kwenye miundombinu mingine.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri