Basilika la Mt. Paulo

Basilika la Kipapa la Mt. Paulo Nje ya Kuta ni mojawapo kati ya mabasilika ya zamani na muhimu zaidi ya Roma[1] pamoja na yale ya Mt. Yohane huko Laterano, Mt. Petro huko Vatikano na Mt. Maria huko Eskwilino.

Upande wa mbele wa Basilika-
Mlango mtakatifu.
Mosaiki ya mwaka 1220 ikimuonyesha Kristo kati ya mitume Petro na Paulo, Mtume Andrea na Mwinjili Luka.
Undani wa kanisa.
Ramani ya basilika
Sibori ya Arnolfo di Cambio.
Mt. Paulo Nje ya Kuta.
Nguzo za nje.

Basilika liko katika eneo la Italia[2], lakini Ukulu Mtakatifu unalimiliki kabisa[3]kama ilivyo kwa maeneo ya balozi za nchi ya kigeni.[4]

Basilika lilianzishwa na kaisari Konstantino Mkuu juu ya mahali (cella memoriae) alipozikwa Mtume Paulo baada ya kukatwa kichwa nje ya ngome ya jiji la Roma.[5][6][7][8][9][10]

Baada ya mabadiliko mengi, lilijengwa upya katika karne ya 19 kwa sababu lilikuwa limeteketezwa na moto. Vipimo vyake ni mita 131.66 kwa 65 kwa 29.70, hivyo ni kanisa la pili kwa ukubwa mjini Roma.

Kumbukumbu ya kutabarukiwa kwake inafanyika kila mwaka tarehe 18 Novemba[11].

Tangu mwaka 1980 Basilika hilo liko katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.

Tanbihi hariri

  1. Benedict XVI’s theological act of renouncing the title of "Patriarch of the West" had as consequence that Roman Catholic patriarchal basilicas are today officially known as Papal basilicas.
  2. Lateran Treaty of 1929, Article 15 (The Treaty of the Lateran by Benedict Williamson (London: Burns, Oates, and Washbourne Limited, 1929), pages 42-66 Archived 23 Mei 2018 at the Wayback Machine.)
  3. Lateran Treaty of 1929, Article 13 (Ibidem Archived 23 Mei 2018 at the Wayback Machine.)
  4. Lateran Treaty of 1929, Article 15 (Ibidem Archived 23 Mei 2018 at the Wayback Machine.)
  5. the earliest account of a visit to the memorials of the apostles is attributed to Gaius, the Presbyter, "who lived when Zephyrinus was bishop of Rome [AD 199–217]", as quoted by Eusebius reporting that "I can point out the tropaia of the Apostles [Peter and Paul]; for if you go to the Vatican or the Ostian Way, you will find the tropaia of those who founded this Church".
  6. "St. Paul's Tomb Unearthed in Rome". National Geographic News. 11 December 2006. Iliwekwa mnamo 21 July 2013.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  7. "St Paul burial place confirmed". Catholic News Agency. 2006-12-06. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-20. Iliwekwa mnamo 2013-03-04. 
  8. "Communiqué about the press conference". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-30. Iliwekwa mnamo 2016-10-07. 
  9. "Associated Press: ''Have St. Paul’s remains been unearthed?''". MSNBC. 2006-12-07. Iliwekwa mnamo 2013-03-04. 
  10. Fraser, Christian (2006-12-07). "Christian Fraser, St Paul's tomb unearthed in Rome, BBC News, 7 December 2006". BBC News. Iliwekwa mnamo 2013-03-04. 
  11. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri