Bavo wa Gent (pia: Baaf, Bavon, Allowin, Bavonius; Hesbaye, Brabant, 622 hivi - Gent, leo nchini Ubelgiji, 1 Oktoba 659 hivi) alikuwa mmonaki, kaka wa Bega na Getrude wa Nivelles[1] .

Mt. Bavo alivyochorwa.

Kabla ya kuongokea maisha maadilifu kwa mahubiri wa Amando wa Maastricht aliwahi kuwa askari na baba wa binti mmoja. Alipofiwa mke wake aliuza mali zake zote kwa ajili ya fukara na kumfuata Amando katika umisionari wake[2].

Baadaye alianzisha monasteri alipoishi hadi kifo chake.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Oktoba[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.