Belarus (kwa Kibelarus: Беларусь (Kikyrili) au Biełaruś (Kilatini); kwa Kirusi:Белоруссия ) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki inayopakana na Urusi, Ukraine, Poland, Lithuania na Latvia.

Belarus
Ramani ya Belarus

Mji mkuu ni Minsk na miji mingine ni pamoja na Brest, Grodno, Gomel, Mogilev na Vitebsk.

Idadi ya wakazi inapungua: ni watu 9,498,700 (2016).

Historia hariri

Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20. Maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Poland, Lithuania na Urusi. Belarus ilikuwa kitengo cha Umoja wa Kisovyet tangu 1919/1922 hadi 1991.

Wakazi na utamaduni hariri

Wakazi walio wengi ni Wabelarus (83.7%) ambao wanaongea ama Kibelarus au Kirusi ambavyo vyote viwili ni lugha rasmi. Lugha hizi mbili zina asili moja. Takriban 11% za wakazi ni Warusi.

Kuna pia vikundi vidogo vinavyotumia lugha za pekee kama vile Kipoland, Kiukraine, Kilatvia, Kilituanya na nyingine.

Walio wengi ni wafuasi wa Ukristo katika Makanisa ya Kiorthodoksi (48.3%) na katika Kanisa Katoliki (7.1%).

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Belarus kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.