Bendera ya Uruguay

Bendera ya Uruguay ina milia ya nyeupe na buluu pamoja ya eneo katika kona ya juu linaloonyesha jua la njano (dhahabu). Idadi ya milia ni tisa kulingana na mikoa ya nchi wakati wa kuanzishwa.

Bendera ya Uruguay

Bendera ina tabia kadhaa za pamoja na bendera ya Argentina: rangi za buluu na nyeupe pia jua la dhahabu. Lakini idadi ya milia ni tofauti pia idadi ya mishale ya jua.

Kuna asili ya pamoja ya kihistoria kwa sababu Argentina na Uruguay zilikuwa zote sehemu za koloni ileile ya Hispania ya Ufalme mdogo wa Rio Plata baadaye ya Maungano ya mikoa ya Río de la Plata (Provincias Unidas del Río de la Plata).