Bijapur ni mji kwenye jimbo la Karnataka katika kusini ya Uhindi. Mji upo kwenye nyanda za juu za Dekkan takriban kilomita 490 kusini-mashariki ya Mumbai na kilomita 470 kaskazini ya Bangalore kwa 16.83 N na 75.71 E. Kuna wakazi 271,064 (2005).

Mji na usultani wa kale wa Bijapur katika Uhundi Kusini
Jengo la Gol Gumbaz mjini Bijapur

Kihistoria Bijapur ilikuwa muhimu kama mji mkuu wa Usultani wa Bijapur kati ya 1490 hadi 1686. Kumbukumbu ya wakati ule ni jengo zuri la Gol Gumbaz lenye kuba kubwa ambalo ni kaburi la sultani pamoja na msikiti.