Burj Dubai (Kiarabu برج دبي‎ - Mnara wa Dubai) ni jengo kubwa la maghorofa linaloendelea kujengwa nchini Dubai (Falme za Kiarabu) tangu mwaka 2004. Litakapokamilika mwaka 2009 litakuwa jengo lenye kimo kikubwa duniani.

Burj Dubai inatarajiwa kufungulia Septemba 2009. Mipango kamili bado ni siri lwa sababu wajenzi wanataka kuwa na uhakika ya kwmaba itakuwa jengo kubwa duniani. Hivyo wameandaa kuongeza ghorofa kama jengo lingine linaendelea kujengwa popote duniani. Kwa sasa inasemekana kuwa na ghorofa 162 na eneo la vyumba vyote ni 334,000 m². Ghorofa ya juu itaishia kwa mita 643 na antenna juu yake itafikia mita 818. Gharama zilipangwa kuwa bilioni za dolari 14.1.

Ghorofa 37 za kwanza zitakuwa hoteli. Juu yake kuna makazi 779 katika ghorofa 38-108 na 700 yameshauzwa. Ghorofa za juu zitakuwa na ofisi na makazi maalumu.

Kutokana na ukubwa na urefu wake Burji khalifa ,husafishwa kwa wiki nane(8).Kihistoria Burj khalifa, ilijengwa kwa ajili ya kuliingizia taifa kipato baada ya mfalme wa falme za kiarabu wa wakati ule kuona hakuna kivutio cha watalii nchini humo.Akaamua lijengwe jengo lefu kuliko yote yote ulimwenguni na wakalipa jina la, BURJ KHALIFA.

Picha za ujenzi hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Burj Khalifa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
 
WikiMedia Commons