Buti (wingi: mabuti; kutoka Kiingereza "boot") ni aina ya kiatu kikubwa kinachofunika mguu pengine hadi magotini. Mara nyingi huwa la ngozi, lakini yale ya kisasa hufanywa kutoka kwa vifaa mbalimbali.

Buti kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi.
Buti zinazotumika maabarani (zinakabiliana na petroli, kemikali za alkali na vitu vingine)
Mwanamke akiwa amevalia mabuti yanayofikia magoti.

Buti huvaliwa kwa kazi maalumu - kulinda mguu kutokana na maji, baridi kali, matope au hatari (kwa mfano, kutokana na kemikali au kutumia vidole vya chuma) au kutoa usaidizi wa ziada wa mguu kwa shughuli zenye nguvu au kwa sababu ya mtindo .

Katika hali nyingine, kuvaa buti kunahitajiwa na sheria au kanuni, kama katika baadhi ya mamlaka zinazohitaji wafanyakazi katika maeneo ya ujenzi kuvaa mabuti ya chuma. Buti linashauriwa pia kwa wapanda pikipiki.

Historia ya buti hariri

Buti za kwanza hazikuwa zimeundwa kama zile za leo. Ilikuwa tu ni mahala pa kukanyagia pamoja na kitambaa kirefu cha kufunika mguu hadi juu ya goti. Miaka ya 1000 KK, buti zilipata sura mpya huku waundaji wakileta ngozi kutoka Asia na kuzitumia kutengeneza buti za ngozi.

Wainuit na Waaleut walitengeneza buti za kuvalia kwa msimu wa kipupwe. Miaka ya 1700, wanajeshi wa Hessian walileta mabadiliko makubwa kwa utengenezaji wa buti maana yao yalionekana marefu yafikayo kwa paja na kwa hiyo ikawa ndio desturi. Watengenezaji wakaunda mabuti marefu ambayo leo kwa Kiingereza yaitwa cowboy boots.

Picha zinazoonyesha historia ya buti huenda zikapatikana vizuri katika mchoro ulioko Hispania unaonyesha mwanamume akiwa amevaa buti za ngozi huku mwanamke akiwa na mabuti ya manyoya. Mchoro huu ulifanyiwa kati ya 12000 na 15000 KK kuonyesha kwamba buti ni vazi la kitambo sana.

Minajili ya uvaaji wa buti hariri

Kwa leo buti huvaliwa na wanaofanya kazi fulani au wale ambao wanatembea katika mazingira fulani kama kwenye maji, tope, theluji au unyevu. Katika mazingira haya, mabuti yafaa isilowe maji au kuingiza ili mvaaji asiende akalowa. Buti pia huweza kuhifadhi joto isiende kwamba mvaaji akapata magonjwa kwa kupata baridi miguuni mwake.

Ulimbwende na utanashati wa kuvaa buti hariri

Mbali na kutumika kwa kazi na kukinga miguu ya mvaaji kutokana na baridi, tope na theluji, buti huvaliwa kwa minajili ya mitindo ya urembo.

Katika sherehe za maonyesho ya mitindo ya uvaaji (fashion shows) buti huvaliwa kuashiria huba na ngono. Wasichana wanaofanya filamu za ngono na huba huwa mara kwa mara wamevaa buti za ngozi, mipira ya PVC au hata latex ili kuweza kuwa na mvuto mkubwa kwa wanaotazama.

Aina za buti hariri

 
Compact British Boots.

Kuna aina nyngi za buti kama vile:

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Buti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.