Bweha (Canis spp.)
Bweha mgongo-mweusi (Canis mesomelas)
Bweha mgongo-mweusi (Canis mesomelas)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Canidae (Wanyama walio na mnasaba na mbwa)
Fischer, 1817
Jenasi: Canis
Linnaeus, 1758
Spishi: C. adustus Sundevall, 1847

C. anthus F. Cuvier, 1820
C. aureus Linnaeus, 1758
C. mesomelas Johann Christian Daniel von Schreber

Bweha au mbweha wa jenasi Canis katika familia Canidae ni wanyama wadogo kiasi wanaofanana na mbwa. Mbwa-nyika (coyote, Canis latrans) huitwa “bweha wa Amerika” pengine[1], lakini kwa kawaida spishi nne tu katika jenasi Canis huitwa bweha.

Spishi hizi huwinda wanyama wadogo hadi wakubwa kiasi, kama mamalia wadogo, ndege na watambaachi. Ili kufanya hiyo husaidiwa na miguu yao mirefu na mikubwa na mifupa ya miguu iliyounganika. Sifa hizi zinawapa bweha uwezo wa kukimbia umbali mrefu na kudumisha mbio za hadi km 16 (maili 9.9) kwa saa kwa vipindi virefu. Bweha hukiakia wakati wa utusitusi wa alfajiri na machweo.

Kwa kawaida sehemu ya kijamii ni jozi inayokaa pamoja abadi na inayokinga eneo lake dhidi ya jozi nyingine wakifukuza washindani wanaovamia na kuweka mkojo na mavi kwa mipaka ya eneo kama landmarks. Ukubwa wa eneo hili unatosha hudhurio la wanyama wazima wachanga ambao wanakaa pamoja na wazazi wao mpaka wanapata maeneo wao. Bweha wanaweza kujikonga katika makundi madogo, kwa mfano ili kula mzoga, lakini kwa kawaida huwinda peke yao au kwa jozi.

Uainishaji na mahusiano hariri

Kwa sababu bweha wa jenasi Canis na mbwa-nyika wanafanana, Lorenz Oken waliwaweka katika jenasi wao wenyewe Thos, kutoka jina la Kiyanuni kwa bweha θώς (Lehrbuch der Naturgeschichte, 1815, juzuu la tatu). Lakini wataalamu wachache wamemfuata.

Angel Cabrera, katika kitabu chake cha 1932 kuhusu wanyama wa Maroko, alijiuliza kwamba kuwepo kwa “cingulum” kwenye magego ya juu ya bweha na kutokuwepo kwa spishi nyingine za Canis kungesadikisha mgawanyiko wa jenasi Canis. Hatimaye alichagua kibadala cha jenasi isiyogawanyika na kurejea bweha kama Canis badala ya Thos[2].

Nadharia ya Oken ilikuwa imefufua mwaka 1914 na Edmund Heller ambaye alisadiki dhana jenasi tofauti. Majina ya Heller na designations alizozipatia spishi na nususpishi za bweha yanaendelea kutumika katika uainishaji wa kisasa ijapokuwa jenasi yao imebadilika tena kuwa Canis.

Tafiti za kisasa zimeonesha mahusiano baina ya spishi za bweha. Licha ya mishabaha yao bweha hawako kwenye tawi moja la mti wa familia Canidae. Bweha miraba na bweha mgongo-mweusi wamo mwenye tawi dhahiri la Canidae, ambapo bweha dhahabu ni karibu na mbwa-mwitu Habeshi (Canis simensis), mbwa-nyika (Canis latrans) na mbwa-mwitu wa Ulaya/mbwa-kaya (Canis lupus)[3]. Kwa sababu bweha miraba/mgongo-mweusi ni tofauti sana na bweha dhahabu (na pia wote wengine wa Canidae wanaofanana na mbwa-mwitu), imependekezwa kubadilisha jina la jenasi ya spishi hizi mbili hadi Lupulella kutoka Canis[4].

Hivi karibuni wataalamu wamefahamu kwamba bweha dhahabu wa Afrika ni spishi tofauti na yule wa Asia na Ulaya[5]. Jina “mbwa-mwitu dhahabu wa Afrika” linapendekezwa kwa spishi ya Afrika.

Spishi hariri

Matumizi ya kale hariri

 
Anubis na mumiani (maiti aliyehifadhiwa)

Mungu wa kale wa Misri, na wa chini duniani, Anubis, aliyezuia maiti wasioze, alionyeshwa kama mwanaume mwenye kichwa cha bweha.

Matumizi ya msimu hariri

 
Bweha dhahabu
  • Taswira maarufu, japo si sahihi sana ya bweha kama wala mizoga kwa kiasi fulani imepelekea tafsiri mbaya.
  • Msemo ”umbweha” wakati fulani hutumika kuelezea kazi ifanywayo na mfanyakazi wa chini kwa ajili ya kuokoa mda ya mtu mkubwa (kwa mfano: mwanasheria mdogo anaweza kufanya kazi nyingi kwa niabu ya wakili). Hii imetokana na ile hadithi ya kwamba bweha humuongoza simba kwenye mawindo yake. Neno hili mli wakati mwingine hutumika kuelezea tabia ya mtu anayependa kujaribu kutumia na kufaidi mizoga ya mtu aliyepatwa na janga fulani. Mfano: kuvamia na kuiba kwenye kijiji kilicho kubwa na mafuriko na wakazi wake wamekimbia.
 
Pundamilia na bweha huko Kasoko ya Ngorongoro, Tanzania

Tanbihi hariri

  1. Coyote (2004) by E.M. Gese & M. Bekoff. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-01-04. Iliwekwa mnamo 2017-04-06.
  2. Thos vs Canis. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-04-16. Iliwekwa mnamo 2017-04-06.
  3. Lindblad-Toh; et al. (2005). "Genome sequence, comparative analysis and haplotype structure of the domestic dog". Nature 438 (7069): 803–819. PMID 16341006. doi:10.1038/nature04338. 
  4. Dinets V. The Canis tangle: a systematics overview and taxonomic recommendations. Vavilovskii Zhurnal Genetiki i Selektsii – Vavilov Journal of Genetics and Breeding. 2015;19(3):286-291.
  5. Koepfli, K.-P.; Pollinger, J.; Godinho, R.; Robinson, J.; Lea, A.; Hendricks, S.; Schweizer, R. M.; Thalmann, O.; Silva, P.; Fan, Z.; Yurchenko, A. A.; Dobrynin, P.; Makunin, A.; Cahill, J. A.; Shapiro, B.; Álvares, F.; Brito, J. C.; Geffen, E.; Leonard, J. A.; Helgen, K. M.; Johnson, W. E.; O'Brien, S. J.; Van Valkenburgh, B.; Wayne, R. K. (2015-08-17). "Genome-wide Evidence Reveals that African and Eurasian Golden Jackals Are Distinct Species". Current Biology 25: 2158–65. PMID 26234211. doi:10.1016/j.cub.2015.06.060.