Cagliari Calcio (maarufu kama Cagliari; matamshi ya Kiitalia: [ˈkaʎʎari]) ni klabu ya mpira wa miguu huko Italia. Klabu hii kwa sasa inacheza katika Serie A.

Uchezaji bora wa klabu hiyo Ulaya ulionekana kwenye mashindano ya kuwania Kombe la UEFA la mwaka 1993-94, ilitolewa na klabu ya Inter milan katika hatua ya nusu fainali.

Historia hariri

Kabla ya Serie A hariri

 
Klabu ya Cagliari (mwaka 1930-1931)

Cagliari walikuwa mabingwa wa kwanza wa Serie C wakati wa msimu wa mwaka 1951-52; kabla ya hapo kwenye ligi, ubingwa ulishirikisha timu zaidi ya moja.

Mnamo miaka ya 1950 Cagliari ilipandishwa Serie B.

Mnamo mwaka 1954 walishushwa na kupelekwa Serie C kwa sababu ya kushuka kiwango cha uchezaji. Baada ya kushuka kwenye Serie C mwanzoni mwa mwaka 1960, Cagliari iliongeza kasi na ubora wa uchezaji na hatimaye ikafanikiwa kupandishwa kwenye Serie A mnamo mwaka 1964.

Uwanja hariri

 
Klabu ya Cagliari ilicheza katika uwanja wa Stadio Sant'Elia mwaka 1970-2017

Klabu ya Cagliari ilihama kutoka katika uwanja wa Stadio Amsicora kwenda katika uwanja wa Stadio Sant'Elia mnamo mwaka 1970, baada ya kushinda taji lao pekee la ligi.

Mizozano na baraza la mji juu ya ukarabati wa uwanja ilimaanisha kuwa Cagliari alicheza michezo yao ya mwisho ya nyumbani ya mwaka 2011-12 huko Stadio Nereo Rocco katika Peninsula ya Italia.

Kwa misimu mingi uliofuata, klabu ya Cagliari ilicheza kwenye uwanja wa Stadio Is Arenas karibu na manispaa ya Quartu Sant'Elena.Uwanja wa Sant'Elia ulibomolewa mnamo mwaka 2017, na kilabu ilihamia uwanja wa Sardegna Arena.

Heshima hariri

Mataji ya kitaifa hariri

  • Serie A:
    • Washindi (1): 1969–1970
  • Serie B:
    • Washindi (1): 2015–2016
  • Serie C / Serie C1:
    • Washindi (4): 1930–1931, 1951–1952, 1961–1962, 1988–1989
  • Coppa Italia Serie C:
    • Washindi (1): 1988–1989
  • Campionato Sardo di I Divisione:
    • Washindi (1): 1936–37

Mataji ya Ulaya hariri

UEFA Cup:

  • Hatua ya nusu fainali (1): 1993–1994

Wachezaji hariri

Kikosi cha sasa( mwaka 2020) hariri

Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.

Na. Nafasi Mchezaji
1   GK Rafael
3   DF Federico Mattiello (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Atalanta B.C.)
4   MF Radja Nainggolan (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Inter Milan)
8   MF Luca Cigarini
10   MF João Pedro
12   DF Fabrizio Cacciatore
15   DF Ragnar Klavan
17   MF Christian Oliva
18   MF Nahitan Nández
19   DF Fabio Pisacane
20   MF Gastón Pereiro
Na. Nafasi Mchezaji
21   MF Artur Ioniță
23   DF Luca Ceppitelli (Kapteni)
24   MF Paolo Faragò
26   FW Daniele Ragatzu
28   GK Alessio Cragno
30   FW Leonardo Pavoletti
33   DF Luca Pellegrini (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Juventus)
34   GK Giuseppe Ciocci
40   DF Sebastian Walukiewicz
43   FW Alberto Paloschi (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya SPAL)
90   GK Robin Olsen (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya A.S. Roma)
99   FW Giovanni Simeone (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Fiorentina)

Barani Ulaya hariri

Kombe la mabingwa wa Ulaya hariri

Msimu Mzunguko Klabu Nyumbani Ugenini Jumla
1970–1971 Mzunguko wa kwanza   Saint-Étienne 3–0 0–1 3–1
Mzunguko wa pili   Atlético Madrid 2–1 0–3 2–4

Kombe la UEFA hariri

Msimu Mzunguko Klabu Nyumbani Ugenini Jumla
1972–1973 Mzunguko wa kwanza   Olympiacos 0–1 1–2 1–3
1993–1994 Mzunguko wa kwanza   Dinamo București 2–0 2–3 4–3
Mzunguko wa pili   Trabzonspor 0–0 1–1 1–1
Mzunguko wa tatu   Mechelen 2–0 3–1 5–1
Robo fainali   Juventus 1–0 2–1 3–1
Nusu fainali   Inter Milan 3–2 0–3 3–5


Tazama pia hariri

Viungu vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: