Charambe ni kata ya Wilaya ya Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 15117.

Kata ya Charambe
Kata ya Charambe is located in Tanzania
Kata ya Charambe
Kata ya Charambe

Mahali pa Charambe katika Tanzania

Majiranukta: 6°52′8″S 39°15′40″E / 6.86889°S 39.26111°E / -6.86889; 39.26111
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Temeke
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 38,587

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 38,587 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 83,401 waishio humo.[2]

Changamoto inayosumbua kata ya Charambe ni umeme na barabara pamoja na kukosekana kwa hospitali.

Tatizo lingine ni msongamano wa nyumba na shule za msingi na sekondari kukosa madarasa na madawati ya kutosha.

Kata ya Charambe ina shule za msingi 4 na shule ya sekondari 1.

Mwaka 2015 katika shule ya Nzasa kulitokea ajali ya mkorosho kangushwa na upepo. Katika ajali hiyo mtoto mmoja aliangukiwa lakini alipona. Maana halisi ya jina la shule Nzasa ni chanzo cha maji.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. 2002 Population and Housing Census General Report (en). Government of Tanzania. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2008-08-21.
  Kata za Wilaya ya Temeke - Tanzania  

Azimio | Buza | Chamazi | Chango'mbe | Charambe | Keko | Kibondemaji | Kiburugwa | Kijichi | Kilakala | Kilungule | Kurasini | Makangarawe | Mbagala | Mbagala Kuu | Mianzini | Miburani | Mtoni | Sandali | Tandika | Temeke | Toangoma | Yombo Vituka