Chombo cha usafiri kwenye maji

Chombo cha majini au chombo cha usafiri kwenye maji ni kitu kinachotumiwa kusafiria kwenye maji kama vile baharini, mtoni au ziwani. Vyombo hivyo vinapatikana vidogo na vikubwa vikiitwa mtumbwi, boti, mashua, mtepe, jahazi au meli; vikitumiwa kuvusha abiria au mizigo kwa umbali mdogo huitwa feri.

Vyombo vya maji vinatofautishwa pia kutokana na jinsi zinavyoendeshwa majini, kwa mfano

Historia

Kihistoria vyombo vya majini vilitengenezwa hasa kwa kutumia ubao au pia mata kavu nyingine kama matete. Tangu karne ya 19 metali, na hasa chuma kilitumiwa kilichoruhusu kujenga meli kubwa.

Katika karne ya 20 mara nyingi aina za plastiki zilichukua nafasi ya ubao kwa vyombo vya majini vidogo zaidi.

Picha

  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.