Chuo Kikuu cha Stellenbosch

Stellenbosch University (awali Chuo Kikuu cha Stellenbosch / Universiteit van Stellenbosch) ni chuo kikuu cha umma cha utafiti katika mji wa Stellenbosch, Afrika Kusini. Vyuo vingine vilivyo karibu ni Chuo Kikuu cha Cape Town na Chuo Kikuu cha Western Cape.

Chuo Kikuu cha Stellenbosch
Universiteit van Stellenbosch
Staff2,430
Wanafunzi26,243
Wanafunzi wa
shahada ya kwanza
15,869
Wanafunzi wa
uzamili
9,233
Mahali{{{mji}}}
RangiMaroon
MsimboMaties
MascotSquirrel[1]
AffiliationsAAU, ACU, CHEC, HESA, IAU
Faili:MatiesLogo.png
Ou Hoofgebou (jengo la zamani la utawala) katika kampasi ya Chuo Kikuu cha Stellenbosch

Stellenbosch University ilisanifu na kuunda microsatellite ya kwanza barani Afrika, SUNSAT, iliyozinduliwa mwaka wa 1999.

Wanafunzi hupewa jina la msimbo Maties . Baadhi wanadai kuwa jina hili linatokana na sare yao ya mchezo wa raga yenye rangi ya maroon: tamatie ni jina la Kiafrikaans la nyanya. Inaelekea zaidi kutoka kwa lahaja ya Kiafrikaans Maat (maana yake "rafiki" au "mwenzi") lililotumiwa sana hapo awali na wanafunzi wa mtangulizi wa Chuo Kikuu cha Cape Town, Chuo cha Afrika Kusini.

Historia hariri

Asili ya chuo kikuu inaweza kufuatiliwa kutoka kwa Stellenbosch Gymnasium , ambayo ilifunguliwa tarehe 1 Machi 1866, na kuwa Stellenbosch College mnamo 1881 na ambayo kwa sasa iliyo katika Idara ya Sanaa. Mwakani 1887 chuo hiki mara renamed Victoria College ; kilipopata hadhi ya chuo kikuu tarehe 2 Aprili 1918 kilibadilishwa jina tena na kuitwa Stellenbosch University .

Jina hariri

Majina yote mawili Chuo Kikuu cha Stellenbosch na Stellenbosch University ni sahihi, ingawa hili la mwisho ndilo rasmi na linapaswa kutumika katika shughuli za kibiashara na mawasiliano. Hii pia inashikilia kweli katika tafsiri za Kiafrikana za jina, na Universiteit van Stellenbosch na Universiteit Stellenbosch [1] Archived 15 Novemba 2010 at the Wayback Machine. [2] Archived 16 Novemba 2010 at the Wayback Machine. Baadhi ya idara hupendelea moja juu ya lingine, kwa mfano, Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Stellenbosch , ambayo hufupishwa kuwa USB .

Daraja hariri

Kulingana na daraja za Chuo Kikuu cha Leiden, SU inaorodheshwa ya 454 katika vyuo vikuu 500 bora duniani kote katika masuala ya uchapishaji kimataifa na ya 415 katika suala la matokeo ya Nukuu kutoka machapisho ya kisayansi ya SU mwaka wa 2007. Hii ni mojawapo ya orodha za kuaminika zaidi katika hadhi ya utafiti lakini haipanii - na kwa sababu nzuri - kuorodhesha vyuo vikuu kwa upana [3] Archived 22 Julai 2011 at the Wayback Machine.

Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Stellenbosch(USB) ilikuwa ya 39 kati ya shule 100 za biashara zinazoongoza duniani, kulingana na utafiti wa Taasisi ya Aspen katika toleo lake mbadala Beyond Pinstripes Grey la 2009-10. USB pia ndio shule ya biashara ya pekee kutoka Afrika Kusini na pia katika bara zima iliyo katika orodha ya 100 bora. [4]

Mwaka 2009 Webometrics iliorodhesha Stellenbosch ya tatu Afrika nyuma ya Chuo Kikuu cha Cape Town na Chuo Kikuu cha Pretoria. [5] Archived 21 Februari 2010 at the Wayback Machine.

Mahali pake hariri

 
Mandhari ya "Red Square" ya Chuo Kikuu cha Stellenbosch kwa upeo, "The Twins"

Stellenbosch, mji mkongwe zaidi nchini Afrika Kusini baada ya Cape Town, ni mji wa chuo kikuu wenye wakazi wapatao 90,000 (ukiondoa wanafunzi). Uko takriban kilomita 50 kutoka Cape Town na uko kwenye kingo za Eersterivier ( "Mto wa Kwanza") katika eneo maarufu kwa ukuzaji wa mvinyo na lililozingirwa na mandhari ya kupendeza ya milima. Mafunzo katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch yamegawanywa kati ya kampasi kuu ya Stellenbosch, kampasi ya Tygerberg, ambapo Kitivo cha Sayansi ya Afya iliko, kampasi ya Bellville Park, ambapo Shule Hitimu ya Biashara iliko, na kampasi ya Saldanha, palipo Kitivo cha Sayansi ya Kijeshi katika Shule ya Jeshi ya Kikosi cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini.

Lugha hariri

Stellenbosch University ni chuo cha kati cha Kiafrikaans, hasa katika vitengo vya shahada za kwanza na za pili. Hata hivyo, wanafunzi wanaruhusiwa kuandika na kufanya kazi zao, majaribio na mitihani katika Kiingereza na Kiafrikana. Lugha ya masomo pia inatofautiana kulingana na Kitivo, Kitivo cha Sanaa kwa mfano kikiwa na asilimia 40 Kiingereza, mafunzo mengi yakifanywa kwa lugha zote mbili na lugha ya takrima au nyenzo nyingi ikidhamiriwa na mwanafunzi.

Katika ngazi ya Uzamili lugha ya masomo hudhamiriwa kwa misingi ya mpangilio wa darasa. Nyingi ya kozi za Uzamili wa juu hufanywa kwa Kiingereza. Kulingana na hali ya sasa, asilimia 60 ya wanafunzi husema kuwa Kiafrikaans ndiyo lugha yao ya nyumbani, asilimia 32 hutumia Kiingereza kama lugha yao ya nyumbani, ilhali asilimia 1.6 tu ya wanafunzi ndio hutumia Kikhosa kama lugha yao ya nyumbani.

Sera ya lugha bado ni suala linaloendelea katika Chuo, kwa kuwa ni mojawapo ya taasisi chache za elimu ya juu katika Afrika Kusini ambazo bado zinatoa mafunzo katika lugha ya Kiafrikana. Kwa sababu hii, kinaenziwa sana katika jamii ya Waafrikana, na hata chuo hiki kuhesabiwa kama nguzo kuu katika maisha ya Kiafrikana. Nyingi ya taasisi zimetoa mafunzo kwa Kiingereza kutoka jadi au kugeuza sera na kuwa za Kiingereza tu.

Wanafunzi hariri

Kirangi, uwakilishi wa wanafunzi katika Stellenbosch University ni kama ifuatavyo:

Usajili Kikabila, 2009 Asilimia Jumla
Wazungu 67.6% 17.753
Machotara 15.2% 4.000
Weusi 14.4% 3.800
Wahindi 1,9% 500
Jumla 100% 26.243

Vitivo na shule hariri

 
kampasi ya Chuo kikuu ya matibabu ya Tygerberg, ikionekana kutoka hewani

Stellenbosch University ina takriban idara 150 katika vitivo 10. Pia ina zaidi ya taasisi 40 za utafiti (na nyinginezo).

Vitivo kwenye kampasi kuu ni:

Vitivo na shule ambazo haziko kwenye kampasi kuu ni:

Vifaa na huduma hariri

Faili:Stellenbosch Student March.jpg
Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Stellenbosch wafanya maandamano na mikutano ya hadhara katika kampasi '

Maktaba ya JS Gericke ni mashuhuri kwa kuwa chini ya ardhi, katika orofa mbili, na kusimama kwenye eneo sawa na nyanja mbili na nusu za mchezo wa raga. Maktaba hii ina mikusanyiko iliyotawanyika kote kampasi nje ya chuo kikuu, na yote imesajiliwa katika hifadhidata ya kompyuta, kwa kutumia kompyuta ya aina ya mainframe asili ya chuo kikuu, aina ya UNIVAC. Kuna maktaba nyingine kadhaa ndogo zinazoshughulikia vitivo mbalimbali, ikiwemo Maktaba ya Thiolojia, Maktaba ya Sheria na Maktaba ya Madaktari ya Tygerberg.

Chuo Kikuu cha Stellenbosch pia kina Mahafadhi pamoja na kumbi mbili za hafla. Mahafadhi hii ndio makao ya Stellenbosch University Choir ambayo imesifika sana kimataifa, pamoja na kuwa kwaya kongwe zaidi Afrika Kusini imepokea tuzo kadhaa ng'ambo[onesha uthibitisho]

Chuo kikuu pia kina ukumbi wa sanaa wenye viti 430, unaojulikana kama HB Thom Theatre na ni ukumbi wazi. Pamoja na vifaa hivi ni idara ya maigizo ya chuo kikuu, chini ya uongozi wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii. Mara kwa mara idara hii hufanya michezo ya kuigiza, makala, kabareti na michezo nyimbo.

Langenhoven Students' Centre (Neelsie) ndio makao ya Halmashauri Wakilishi ya Wanafunzi, ukumbi wa maankuli, senema, ofisi ya posta, kituo cha manunuzi, ofisi ya ushauri na ofisi za vilabu vyote vya mwanafunzi. Bendi za wanafunzi na shughuli mbalimbali za burudani kwa kawaida hufanyika katika ukumbi wa maankuli wakati wa chakula cha mchana.

Chuo hiki kina redio yake inayojulikana kama MFM (Matie FM), iliyo na kikao chake katika Neelsie. Hupeperusha matangazo katika eneo lote la Stellenbosch katika mitabendi 92.6 FM. Hupeperusha mchanganyiko wa muziki, habari, burudani na habari za kampasi.

Chuo hiki pia husambaza machapisho kama vile Die Matie (linaloonekana kila baada ya wiki mbili), kwa ajili ya wanafunzi wake na Kampusnuus (kila mwezi) kwa wafanyakazi wake. Yearbook rasmi, Die Stellenbosch Student , huchapishwa kila mwaka na kupewa kwa wanafunzi wote waliofuzu. Matieland ni jina la gazeti rasmi la wanafunzi wa zamani. Huchapishwa mara mbili kwa mwaka na kusambazwa kwa baadhi ya wanfunzi 100,000 wa zamani na marafiki wa Chuo Kikuu.

Michezo hariri

Vifaa vya michezo kwa zaidi ya nyanja 30 za ushindani na burudani za michezo zinaungwa mkono na chuo kikuu pamoja na viwanja viwili vya michezo, mabwawa mawili makubwa ya kuogelea (chini ya paa moja), na DF Malan Center, ukumbi wa kusudi mbalimbali kama sherehe na michezo ya ndani, viwanja vingi vya kuchezea, kikiwemo cha Hockey, na pumzikio. Chuo kikuu hutoa michezo ifuatayo kwa wanafunzi wake:

Mwaka wa 2006 Stellenbosch ilikuwa kituo cha kujaribia mapendekezo kahdaa katika sheria za shirikisho la raga, zinazojulikana kama Sheria za Stellenbosch.

Makazi ya wanafunzi hariri

Chuo hiki kina makazi mbalimbali au kwa jina lingine koshuise (jina la Kiafrikana la kumbi za makazi).

Wanafunzi katika mabweni ya binafsi wanaweza kuwa wanachama wa Private Students' Organisation (PSO), inayojulikana pia kama Private Wards. Awali kulikuwa PSO 6 hadi 8 Oktoba 2008, wakati PSO nne mpya zilipofunguliwa. Wanafunzi hupewa makao mbalimbali kupitia mfumo wa mgao wa bahati nasibu. Makao ya kibinafsi huruhusu wanafunzi wote kufurahia utendaji sawa, kutoka misaada ya kitaaluma, nafasi za kimichezo, kama zinazotolewa na makao ya chuo, ilhali mwanafunzi akibakia katika makaazi ya kibinafsi.

Wanafunzi wa Zamani Mashuhuri hariri

Marejeo hariri

  1. "Meet Pokkel the Maties mascot", Matie News, 18 Februari 2009

Viungo vya nje hariri

Coordinates: 33°55′48.27″S 18°51′53.01″E / 33.9300750°S 18.8647250°E / -33.9300750; 18.8647250