Dismas Mtakatifu ni jina lisilo na hakika la mhalifu aliyesulubiwa pamoja na mwenzake na Yesu kwa amri ya Ponsyo Pilato.

"Kristo na Mhalifu" kadiri ya Nikolai Ge.

Habari hii inasimuliwa na Injili zote (Math 27:38; Mk 15:27-28,32; Lk 23:33; Yoh 19:18) lakini ni Luka tu anayesema kuwa, kati ya hao wawili waliokuwa msalabani kandokando ya Yesu, mmoja alitubu na kumuomba kwa imani, "Ee Yesu, unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako".

Yesu hakuchelewa kumjibu: "Kweli nakuambia, leo hii utakuwa nami katika paradiso".

Ndiyo sababu Wakristo wengi wanamheshimu kama mtakatifu, hasa tarehe 25 Machi[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dismas Mtakatifu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.