Jina la kikoa

(Elekezwa kutoka Domain name)

Jina la kikoa ni jina ambalo ni kama kitambulisho na linafafanua ulimwengu wa utawala, uhuru mamlaka wa wavuti fulani katika mitandao.

Jina la kikoa hutengenezwa na katiba na utaratibu wa DNS. Jina lolote lililoandikishwa ndani ya DNS ni jina la kikoa .

Kwa ujumla, jina la kikoa hutambulisha anwani ya IP, kama vile tarakilishi ya binafsi ambayo hutumika katika upatikanaji wa intaneti.

Kufikia mwaka 2017, majina ya kikoa milioni 330.6 yailiandikishwa.

Mapendekezo ya jina la kikoa hariri

Jina la kikoa huwa na jina la biashara au shirika unalofanya kazi nalo ambalo ungetaka liwe na wavuti. Kwa mfano, jina kama 'Kiswahilikitukuzwe.org' linaashiria kuwa utakuwa ukijadili maswala ya kiswahili na hilo ni shirika kwa sababu ya jinsi kikoa chenyewe kinavyoisha kwa .org.

Majina ya kikoa ya kibiashara huishia kwa '.com'. Huenda pia domain ikawa inaashiria mahala hilo shirika au biashara ipo kwa mfano .or.tz kuonyesha kuwa ii katika nchi ya Tanzania.