Domnio (pia: Dujam, Duje, Doimus na Domninus; Antiokia, leo nchini Uturuki, karne ya 3 - Salona, leo Solin nchini Kroasya, 304) alikuwa askofu wa Salona aliyeuawa kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya Dola la Roma kwa sababu ya imani yake[1].

Mt. Domnio akishika mkononi mji wa Split.

Inasemekana aliuawa pamoja na Wakristo wengine 7 wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 11 Aprili[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.