Edmundi Gennings (Lichfield, Uingereza, 1567London, 10 Desemba 1591) alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki.

Mt. Edmundi.

Baada ya kuhamia Ufaransa, aliingia seminari kwa lengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali, akapewa daraja ya upadri (1590).

Hapo alirudi London lakini baada ya muda mfupi aliuawa kwa kunyongwa kikatili na kukatwa vipandevipande chini ya sheria.

Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39.

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.