Encyclopedia Iranica

Encyclopædia Iranica ni kamusi elezo ya kitaalamu kuhusu historia, utamaduni, na ustaarabu wa watu wa Iran.

Ilianzishwa mwaka 1973 na profesa Ehsan Yarshater ikisimamishwa na taasisi ya Center for Iranian Studies kwenye Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York.

Kamusi elezi hiyo inalenga kukusanya elimu ya kitaaluma kuhusu Iran wa leo lakini pia kuhusu maeneo yote yaliyokuwa sehemu za dunia ya Kiajemi katika historia. na uhusiano baina ya Uajemi na tamaduni nyingine kama vile China na Ulaya.[1] [2] Mradi unapanga kuchapisha jumla ya majuzuu 45 lakini tangu mwanzo maudhui yote inapatikana pia katika intaneti kupitia tovuti iranicaonline.org.

Marejeo hariri

  1. Boss, Shira J. (November 2003). "Encyclopedia Iranica". Columbia College Today. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-18. Iliwekwa mnamo 2016-07-14.  Check date values in: |date= (help)
  2. Trompf, Garry W. (2008). "Encyclopedia Iranica - 35: A New Agenda for Persian Studies?". Iran & the Caucasus 12 (2): 385–395. JSTOR 25597382. doi:10.1163/157338408X406137. 

Viungo vya nje hariri