Eneo bunge la Westlands


Eneo bunge la Westlands ni eneo la uchaguzi nchini Kenya. Ni mojawapo kati ya maeneo bunge kumi na saba ya Kaunti ya Nairobi. Eneo la bunge hili lote liko ndani ya eneo la Baraza la Mji wa Nairobi. Lilikuwa linajulikana kama Eneo bunge la Kaskazini mashariki mwa Nairobi katika uchaguzi wa mwaka wa 1963,kisha kama Eneo bunge la Parklands na tangu uchaguzi wa mwaka wa 1988, limejulikana kama eneo bunge la Westlands.

Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi

Eneo bunge la Westlands lina baadhi ya maeneo ya mapato ya juu mjini Nairobi, vilevile maeneo duni kama Kangemi.

Wabunge hariri

Mwaka wa Uchaguzi Mbunge [1] Chama Vidokezo
1963 Fitz Remedios Santana de Souza KANU
1969 Samuel Kivuitu KANU Mfumo wa chama kimoja
1974 Isaac Waweru KANU Mfumo wa chama kimoja
1979 Krishan Chander Gautama KANU Mfumo wa chama kimoja
1983 Samuel Kivuitu KANU Mfumo wa chama kimoja.
1988 Njoroge Mungai KANU Mfumo wa chama kimoja.
1992 Amin Walji KANU Walji alifariki akiwa mbunge[2]
1994 Fred Gumo KANU Uchaguzi mdogo
1997 Fred Gumo KANU
2002 Fred Gumo NARC
2007 Fred Gumo ODM Gumo 35,821; Tett 24,594; Mueke 5501; Pattni 4586

Tarafa na kata hariri

Kata
Tarafa Idadi ya Watu
Highridge 65,268
Kangemi 82,964
Kilimani 61,290
Kitisuru 38,424
Lavington 26,540
Parklands 16,031
Jumla x
Septemba 2005 | [3]Civic Elections Results (2005)
Kata
Wadi Wapiga kura waliosajiliwa
Highridge 26,875
Kangemi 24,239
Kileleshwa 17,064
Kilimani 29,684
Kitisuru 17,143
Parklands 20,114
Jumla 135,119
Septemba 2005 | [3]

Marejeo hariri

  1. Center for Multiparty Democracy:Politics and Paliamenterians in Kenya 1944-2007 Archived 28 Februari 2008 at the Wayback Machine.
  2. [1] ^ Daily Nation, 18 Machi 2002: Mwau akitazama uchaguzi wa miunganao uliopita
  3. 3.0 3.1 Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency

Viungo vya nje hariri