Espero, Zoe na wanao

Espero, Zoe na wanao (walifariki Atalia katika Pamfilia, leo nchini Uturuki, 127 hivi) walikuwa Wakristo watumwa wa Mpagani, ambao huyo alidai wateswe na hatimaye kuchomwa moto katika tanuru kwa sababu walikiri wazi imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Hadrian wa Dola la Roma.

Espero na Zoe walikuwa mume na mke kutoka Italia, Kiriako na Theodulo watoto wao[1][2][3].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao ni tarehe 2 Mei[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.