Eternal lilikuwa kundi la wasichana wa Kiingereza wanaoimba muziki wa R&B. Kundi limeanzishwa mwaka 1992 likiwa na ndugu kina Easther na Vernie Bennett, Kéllé Bryan na Louise Nurding. Kundi limepata mafanikio kimataifa, kwa kuuza nakala milioni 10 dunia nzima. Nurding ameondoka mwaka 1995 na kwenda kufanya kazi za kujitegemea kwa mafanikio tele. Bryan alivutwa mnamo 1998 na wanachama wengine wawili, ambao walidai wameondoka kwa sababu ya mahusiano kitaalamu tu. Waliobakia waliachana mwaka 2000. Walihesabiwa kama jibu la Uingereza kwa kundi la kike la Kimarekani En Vogue.[1][2]

Eternal
Taarifa za awali
ChimbukoLondon, Uingereza
AlaSauti
Miaka ya kazi
StudioEMI
Wanachama wa zamani

Albamu ya kwanza ya Eternal Always & Forever (1993) ilishika nafasi ya pili kwenye chati za UK Album Chart na kwenda kupata platinamu nne huko nchini Uingereza. Mwaka wa 1997, walifika nafasi ya kwanza kwenye chati za UK Singles Chart na kibao chao cha "I Wanna Be the Only One", ambacho kiliwapatia ushindi katika tuzo za Mobo Award 1997 ikiwa kama Single Bora. Vilevile walipata kuchaguliwa mara saba kwenye tuzo za Brit Award - lakini hawajashinda. Kwa ujumla wamefanikiwa kufikia 15 hadi 20 bora nchini Uingereza kuanzia 1993 hadi 1999, huku wakiwa na 10 bora zao kwa vibao kama vile "Stay" (1993), "Oh Baby I..." (1994), "Power of a Woman" (1995), "Someday" (1996), "Secrets" (1996) na "Don't You Love Me" (1997). Mwaka wa 2013, kundi liliundwa upya wakiwa watatu bila Louise Redknapp kwa ajili ya mfululizo wa pili wa kipindi cha TV kupitia runinga ya ITV2 The Big Reunion, na kutumbuiza katika tamasha moja tu mnamo mwezi Machi 2014.[3]

Kazi hariri

Members hariri

Mwanachama 1992 1993 1994 1995 1996 1997 1998 1999 2000 2013 2014 2015
Easther Bennett
(1992–2000, 2013–hadi sasa)
Vernie Bennett
(1992–2000, 2013–hadi sasa)
Kéllé Bryan
(1992–1998, 2013–2014)
Louise Nurding
(1992–1995)
  • Tanbihi: hao walio kwenye maandishi yaliyokoozwa ni wanachama wa sasa.

Diskografia hariri

Albamu za studio hariri

Albamu za kompilesheni hariri

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri

Kigezo:Eternal