Eustasi wa Luxeuil

Eustasi wa Luxeuil (560 hivi – 629 hivi), alikuwa abati wa pili wa Luxeuil kuanzia mwaka 611, akimrithi mwalimu wake Kolumbani, baada ya kuwa mkuu wa chuo cha monasteri.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa hasa tarehe 2 Aprili[1].

Maisha hariri

Eustasi alizaliwa huko Burgundy (leo nchini Ufaransa) akatawa huko Luxeuil.

Kolumbani, mwanzilishi wa abasia hiyo, alipofukuzwa na mfalme wa Burgundy kwa sababu ya kukemea maadili yake, alimpendekeza Eustasi achaguliwe kushika nafasi yake, akahamia Bobbio, Italia.[2][3]

Eustasi alikuwa mtu mnyenyekevu, wa sala na mfungo wa kudumu.

Chini yake, monasteri ilizidi kusifiwa kwa elimu na utakatifu wa wamonaki wake 600. Pamoja na baadhi yao alijitosa kuhubiri maeneo yasiyoinjilishwa bado, hasa katika Galia ya kaskazini-mashariki, lakini pia Bavaria. Wengine wakawa maaskofu na watakatifu.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.