41°00′47″N 24°17′11″E / 41.01306°N 24.28639°E / 41.01306; 24.28639

Ramani ya Ugiriki ikionyesha Filipi.
Vyombo vilivyopatikana Filipi.
Basilika B.
Jina la askofu Porphyrios katika Basilika la Mt. Paulo.
Mabaki ya kanisa kuu.

Filipi (kwa Kigiriki Φίλιπποι, Philippoi) ulikuwa mji wa Makedonia ya mashariki, ulioanzishwa na Filipo II wa Makedonia mwaka 356 KK ukaachwa katika karne ya 14 kutokana na uvamizi wa Waturuki.

Leo kuna Filippoi tena karibu na magofu ya mji wa zamani katika mkoa wa Makedonia ya mashariki na Thrakia nchini Ugiriki.

Katika Biblia hariri

Kadiri ya Agano Jipya, mwaka 49 au 50 mji ulitembelewa na Mtume Paulo kutokana na njozi aliyoipata ikiwa na himizo la kuingia Ulaya ili kuwaletea Injili Wamakedonia (Mdo 16:9-10).

Matendo ya Mitume kinasimulia hivi: 16:11 Basi tukang’oa nanga kutoka Troa, tukafika Samothrake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli; 12 na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. 13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. 14 Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo. 15 Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatushurutisha.

Paulo alidumisha uhusiano mzuri na jumuia ya Kikristo aliyoweza kuianzisha huko kwa muda mfupi, akaitembelea tena mwaka 56 na 57.

Waraka kwa Wafilipi uliweza kuandikwa miaka 61-62.

Marejeo hariri

  • Ch. Bakirtzis, H. Koester (ed.), Philippi at the Time of Paul and after His Death, Harrisburg, 1998.
  • P. Collart, Philippes ville de Macédoine de ses origines jusqu'à la fin de l'époque romaine, Paris, 1937.
  • G. Gounaris, E. Gounaris, Philippi: Archaeological Guide, Thessaloniki, 2004.
  • P. Lemerle, Philippes et la Macédoine orientale à l'époque chrétienne et byzantine, Ed. De Boccard, Paris, 1945.
  • M. Sève, "De la naissance à la mort d'une ville : Philippes en Macédoine (IVe siècle av. J.-C.–VIIe siècle apr. J.-C.)", Histoire urbaine n° 1, juin 2000, 187–204.
  • Ch. Koukouli-Chrysanthaki, Ch. Bakirtzis, Philippi Athens, second edition, 1997.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ugiriki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Filipi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.