George Gershwin (26 Septemba 189811 Julai 1937) alikuwa mtungaji wa muziki na mpiga kinanda kutoka nchi ya Marekani. Alitunga nyimbo nyingi zilizoathiriwa na mitindo ya Jazz. Pia alitunga opera moja iitwayo Porgy na Bess. Aliaga dunia mapema baada ya kupatwa na kansa ya ubongo. Mwaka wa 1998 alituzwa tuzo maalumu ya Tuzo ya Pulitzer ya Muziki kwa kazi ya maisha yake, yaani baada ya kifo chake.


Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu George Gershwin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.