Gregor Johann Mendel (Heinzendorf bei Odrau, Milki ya Austria, leo Hynčice nchini Ucheki, 20 Julai 1822Brünn, Austria-Hungaria, leo Brno, Ucheki, 6 Januari 1884) alikuwa mmonaki, padri wa Kanisa Katoliki na hatimaye (1867) abati.

Padri Gregor Mendel katika sare ya kimonaki
Abasia ya Mt. Thomas, Brno
Tabia thabiti na tabia dhaifu (1) Kizazi cha wazazi (2) kizazi cha F1 (3) kizazi cha F2

Mtaalamu wa botania na hisabati,[1] ni maarufu kimataifa hasa kama mwanzilishi wa elimu ya jenetikia kutokana na utafiti wake kuhusu njegere. Alitambua mfumo wa urithi wa tabia thabiti na tabia dhaifu. Mfumo huu aliueleza kwa mafundisho yanayojulikana leo kama sheria ya urithi ya Mendel.

Maisha hariri

Johann Mendel alizaliwa katika familia ya wakulima[2] wa Kijerumani huko Heinzendorf bei Odrau, Silesia, Milki ya Austria. Jina Gregor alipewa alipojiunga na Waaugustino mwaka 1843.[3]

Kabla ya hapo, wakati wa masomo yake ilimbidi mara kadhaa kuyasimamisha kutokana na ugonjwa, mbali ya matatizo ya uchumi.[4]

Alipata upadrisho tarehe 6 Agosti 1847.

Mwaka 1851 alitumwa kusoma katika Chuo Kikuu cha Vienna chini ya Abati C. F. Napp[5] akiwa na Christian Doppler kama mwalimu wa fizikia.[6]

Mendel alirudi monasterini mwaka 1853 kama mwalimu, hasa wa fizikia.[7]

Pia alisoma astronomia na meteorolojia,[8] akianzisha 'Shirika la Meteorolojia ya Austria' mwaka 1865.[6] tena vitabu vyake vilivyochapwa vinahusu zaidi fani hiyo ya mwisho.[6]

Mwaka 1867 alishika nafasi ya Napp kama abati[8], na hivyo kupungukiwa nafasi kwa utafiti wake wa kisayansi·[9]

Mendel alianza kufanya utafiti kuhusu urithi wa umbile kwa kutumia kwanza panya, halafu mimea.[10]

Mendel alifariki tarehe 6 Januari 1884, akiwa na umri wa miaka 61, kwa nephritis ya kudumu.

Utafiti wake wa njegere hariri

Mendel alitumia njegere zenye tabia mbalimbali: kwa mfano aina fupi na ndefu, zenye rangi ya njano au kibichi, zenye maua ya rangi tofauti.

Akizalisha aina hizi kwa kuzichanganya aliona ya kwamba kizazi cha pili cha mchanganyiko kilionyesha tabia moja tu, maana tabia thabiti ilishinda na tabia dhaifu haikuonekana tena. Lakini alipoendelea kuzalisha njegere za kizazi cha pili matokeo katika kizazi cha tatu zilikuwa tofauti. Hapa tabia dhaifu ilitokea tena.

Mendel aliendelea kuzalisha njegele na kuandika takwimu jinsi gani tabia tofauti zilitokea katika vizazi vya pili na vya tatu. Aliona mwanzoni ya kwamba katika kizazi cha tatu 3/4 zilionyesha tabia thabiti na robo 1 tabia dhaifu. Lakini alipoendelea kuzalisha katika kizazi kifuatacho alijifunza ya kwamba robo mbili ziliendeleza tabia 1 tu (ama ndefu au fupi n.k.) na nusu iliyobaki iliweza tena kuleta tabia zote mbili katika kizazi cha baadaye. Kwa hiyo katika kizazi hiki robo mbili zilikuwa safi kitabia na nusu ilikuwa na tabia chotara.

Hapo aligundua ya kwamba tabia zinaendelezwa kwa kipimo cha 1:2:1 yaani 1 safi A : 2 chotara AB : 1 safi B.

Hapo ilithibitika ya kwamba katika kuzalisha tabia tofauti hizi hazichanganyikana tu lakini bado zote mbili zilikuwepo na kutokea katika vizazi vya baadaye. [11][12][13]

Mendel aliandika kitabu juu ya utafiti wake mwaka 1866 lakini wakati ule watu hawakuelewa bado umuhimu wake.

Jenetikia ya kisasa ilianza miaka 35 baadaye wakati kazi za Mendel zilisomewa tena. Hivyo sifa ilimfikia tu baada ya kufa.[14]

Tanbihi hariri

  1. "Gregor Mendel". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2007-4-4.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Gregor Mendel, Alain F. Corcos, Floyd V. Monaghan, Maria C. Weber "Gregor Mendel's Experiments on Plant Hybrids: A Guided Study", Rutgers University Press, 1993.
  3. Henig|2000|p=24
  4. Henig|2000|pp=19–21
  5. Henig|2000|pp=47–62
  6. 6.0 6.1 6.2 "The Mathematics of Inheritance". Online museum exhibition. The Masaryk University Mendel Museum. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-03-15. Iliwekwa mnamo 20 January 2010.  Check date values in: |accessdate= (help)
  7. Henig|2000|pp=47–62
  8. 8.0 8.1 "Online Museum Exhibition". The Masaryk University Mendel Museum. Iliwekwa mnamo 20 January 2010.  Check date values in: |accessdate= (help)
  9. Windle, B.C.A.; Translated Looby, John (1911). "Mendel, Mendelism". Catholic Encyclopedia. Iliwekwa mnamo 2 April 2007.  Check date values in: |accessdate= (help)
  10. Henig|2000|pp=15–17
  11. Stern, Curt and Sherwood, Eva R. (eds) 1966. The origin of genetics: a Mendel source book. Freeman, S.F.
  12. Carlson, Elof Axel 1966. The gene: a critical history. Saunders.
  13. Olby, Robert 1985. Origins of Mendelism, 2nd ed. Chicago.
  14. Henig, Robin Marantz 2000. A monk and two peas: the story of Gregor Mendel and the discovery of genetics. Weidenfeld & Nicolson, London.

Marejeo hariri

  • Iltis, Hugo 1932. Life of Mendel, transl. by Eden & Cedar Paul. Allen & Unwin, London. German original: Gregor Mendel: Leben, Werk und Wirkung. Springer, Berlin 1924.

Viungo vya nje hariri