Hifadhi ya Taifa ya Mudumu

Hifadhi ya Taifa ya Mudumu, ni hifadhi ya taifa katika Mkoa wa Caprivi kaskazini mashariki mwa Namibia . Hifadhi hiyo ilianzishwa mnamo 1990. Inachukua eneo la kilomita za mraba 737. Mto Kwando unaunda mpaka wa magharibi na Botswana . Hifadhi mbalimbali za maeneo ya jumuiya na misitu ya jamii yanazungukwa na hifadhi ya taifa ya Mudumu. [1]

Hifadhi ya Taifa ya Mudumu
Hifadhi ya Taifa ya Mudumu

Eneo hili ni njia muhimu ya uhamiaji kutoka Botswana hadi Angola kwa wanyama wakubwa kama vile tembo wa Kiafrika . [2] [3]

Historia hariri

Mbuga ya taifa ya Mudumu ilianzishwa mwaka 1990, muda mfupi kabla ya uhuru wa Namibia . [4] Ingawa saizi iliyoidhinishwa ya mbuga hiyo ni kilomita za mraba 1,010, ila ukubwa halisi ni kilomita za mraba 737. [5]

Marejeo hariri

  1. State of Protected Areas in Namibia. Windhoek, Namibia: Ministry of Environment and Tourism, Namibia. 2010. uk. 172. 
  2. . Windhoek, Namibia: Ministry of Environment and Tourism. 2009. uk. 4.  Missing or empty |title= (help)
  3. Draft management plan for Mudumu National Park. Windhoek, Namibia: Ministry of Environment and Tourism. 2012. uk. 58. 
  4. . Windhoek, Namibia: Ministry of Environment and Tourism. 2009. uk. 4.  Missing or empty |title= (help)
  5. State of Protected Areas in Namibia. Windhoek, Namibia: Ministry of Environment and Tourism, Namibia. 2010. uk. 172.